Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amewaapisha Viongozi Aliowachagua hivi karibuni

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi aliowateuwa hivi karibu, hafla hiyo ya kuwaapishwa iliyofanyika leo 4-7-2022 Ikulu Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi  Dk. Hussein Mwinyi amewataka watendaji wa Wizara za Serikali kufanya kazi kwa bidii, mashirikiano na kuaminiana ili kuwatumikia Wazanzibari ipasavyo.

Dk. Mwinyi ametoa wito huo katika hafla ya kuwaapisha Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, aliowateuwa Juni 30, 2022.

Amesema pamoja na mambo mengine uteuzi wa watendaji hao umezingatia sababu kuu mbili, ikiwemo ile ya baadhi ya watendaji wa Wizara hizo kufanya kazi bila maelewano na hivyo kukosekana ufanisi.

Alisema amewarejesha Ma Naibu Katibu Wakuu wa Wizara za Serikali  Awamu ya saba kuendelea na nyadhifa hizo kwa lengo la kuwaongezea nguvu Makatibu wakuu kutokana na kuzidiwa mno na majukumu sambamba na kazi kutetereka pale watendaji hao (Makatibu wakuu) wanapokuwa hawapo.

“Hakukuwa na sababu ya kuteuwa watendaji wapya ..... ni matarajio yangu hawa waliokuwa katika awamu ya saba watatenda vyema”, alisema.

Aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa bidii na kuahidi kuwapandisha vyeo watendaji wote watakaotekeleza vyema majukumu yao ya kazi.

Katika hatua nyengine; baadhi ya Ofisi na Wizara za Seriklai  ikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ hazikufikiwa na mabadiliko na uteuzi huo.

Aidha, taasisi nyingine ambayo haikufikiwa na mabadailiko na uteuzi huo ni Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Katika hafla hiyo, viongozi mbali mbali wa Kitaifa  walihudhuria, akiwemo Mkaamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Mwinyi Talib Haji, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said.

Wengine ni pamoja na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Viongozi wa Dini, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wanafamilia.  

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Nadir Abdullatif Yussuf, kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo 4-7-2022.
BAADHI ya  Wanafamilia na Wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi aliowachagua hivi karibuni hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo 4-7-2022.
WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi aliowachagua hivi karibuni, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo 4-7-2022.
VIONGOZI Wakuu wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibuni (kutoka kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdalla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi aliowaapisha leo 4-7-2022 Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.