Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Kiongozi Mkuu wa Bohora (Dawoodi Bohoras) Ikulu.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya mazungumzo na kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras) duniani, Syedna Muffaddil Saifuddin na kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa dhehebu hilo kuja kuekeza Zanzibar.

Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Zanzibar ambapo kiongozi huyo wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras), akiwa na ujumbe wake walionesha azma ya kuendedelea kumuunga mkono Rais Dk. Mwinyi katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo Rais Dk. Mwinyi alimueleza kiongozi huyo fursa mbali mbali zilizopo Zanzibar pamoja na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayoiongoza katika biashara na uwekezaji.

Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa dhehebu hilo kubwa duniani kuja kuekeza Zanzibar na kuwahakikishia kwamba Serikali imeweka mikakati madhubuti sambamba na mashirikiano makubwa.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano,

Ikulu Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.