Habari za Punde

Wizara ya Fedha na Mipango ni moja ya washiriki katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Maonesho ya Sabasaba.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu idara ya uchambuzi wa sera kutoka kwa Mchumi Bi. Jesca Mugyabuso kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pindi alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu Mfumo wa Kieletroniki wa Ulipaji wa Huduma za Serikali (GePG) kutoka kwa Afisa Tehama Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Kifedha Bw. Zuberi Msisi, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.  
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu Taasisi ya UTT AMIS kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Taasisi hiyo Bi. Martha Mashoku, pindi alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam  
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akimsikiliza kwa umakini Mhadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bw. Christopher Mdoe,  pindi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam  
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akimsikiliza kwa umakini Mhitimu na Mjasiramali kutoka Chuo cha Uhasibu (TIA) Bw. Isaya Maligite, pindi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango ni moja ya washiriki katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Maonesho ya Sabasaba.

Katika maonesho hayo Wizara, imeshiriki pamoja na  baadhi ya Taasisi zake zikiwemo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT- AMIS, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Tanzania Commercial Bank( TCB), Hazina Saccos, Mfuko wa Self, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA),  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). 

Wizara na Taasisi zake inashiriki katika maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa umma. Maonesho haya ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yalianza rasmi tarehe 28 Juni 2022, yanatarajiwa kufungwa 13 Julai, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.