Habari za Punde

Ajali ya Gari Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo na Kujeruhi Wanafunzi Watu na Mmoja Kufariki Katika Ajali hiyo.

Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kupitia kitengo cha Huduma za Dharura kimepokea majeruhi 3 na maiti ya mtoto mmoja katika Ajali iliyotokea leo majira ya asubuhi huko Kitope Muembe Majogoo basi la wanafunzi la Skuli ya Focus Vission Islamic School, lililokuwa likielekea kazole Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo 18-8-2022.

Majeruhi hao wamepokelewa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja majira ya saa nne (4) za za asubuhi na wanaendelea na matibabu kwa haraka zaidii.

Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Naibu Waziri wa Afya Zanzibae Mhe.Hassan Khamis Hafidh pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe , Ali Abdulgulam Hussein wamefika hospitali kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji majeruhi hao.
 
Taarifa kutoka kwa mkuu wa Devisheni Kitengo cha Huduma za Dharura Dk, Tatu Khamis Hussein. 

Habari kamili tutawajuulisha baadae.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.