Habari za Punde

Wazazi watakiwa kuwahimiza watoto kusoma Madrasah

 Na  Kijakazi Abdalla           26/11/2022

Wazazi wametakiwa kuwapa fursa watoto wao kusoma masomo ya madrasa ili kupata kukijua kitabu cha Mwenyezimungu pamoja na makatazo yake badala ya kusoma masomo ya kidunia pekee.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni,Vijana na Michezo ,Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar  Dkt. Mwanahija Ali Juma katika sherehe ya Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Al-Madrasatul-raudwa Kibweni Zanzibar.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wazazi kutowapa fursa watoto kusoma masomo ya chuoni na kuwaruhusu zaidi watoto kushughulikia masomo ya dunia pekee.

Aidha amesema watoto wanapokuwa darasa la kwanza hadi la saba ni vyema kwa watoto kuwalea zaidi nyumbani  badala ya kuwapeleka zaidi katika makambi hali hiyo husababisaha watoto kutozingatia masomo ya madrasa.

Vilevile Katibu huyo amewaasa wazazi kutoa fursa sawa kwa watoto wa kiume kusoma madrasa na kuacha tabia ya kuwaruhusu kukaa vijiweni zaidi kwani hali ambayo inawadumaza kiakili kwa vile wao ndio wachunga zaidi katika kuongoza familia.

 Mapema wakisoma risala Uongozi wa Madrsatul Raudwa wamesema chuo kinakabiliwa na changamoto ya utoro kwa baadhi ya wanafunzi pamoja na kubanwa zaidi wanafunzi kwa masomo ya ziada maskulini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.