Habari za Punde

Tumuunge mkono Rais kwenye vita dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia nchini

 

Na Maulid Yussuf

Mkurgenzi wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii ndugu Sitti Abass Ali amewataka washiriki wa mkutano wa jukwaa maalum kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi katika mapambano ya kupunguza vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia nchini. 

Amesema hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Zura ulioko mkoa wa mjini Unguja, wakati wa mkutano wa jukwaa maalum wa majadiliano kwa ajili ya ushughulikiaji wa matukio na kesi za udhalilishaji nchini.

Aidha amewataka maafisa hao kujua wajibu na lengo la kuundwa juukwaa hilo kwa ajili ya kupunguza matendo hayo nchini.
"Tunapaswa kujua wajibu na malengo, tumeona umuhimu wa kuwepo hichi kikosi kazi chenye uzoefu na weledi wa kupambana na udhalilishaji nchini". alieleza Sitti Abass.

Ndugu Sittti amewasisitiza maafisa kujadili kesi na taarifa zilizopo zinasimamiwa kwa wakati ili waathirika kuweza kupatiwa haki zao.

Vilevile amezitaka taasisi za One Stop Centre, Jeshi la Polisi, Mahakama na zengine kuendeleza mashirikiano na Wizara ya Maendeleo ili kuwasaidi Wanawake na Watoto.

Mapema washiriki wa kikao hicho wamependekeza kuwepo kwa wakuu wa vitengo katika vikao vya kupinga udhalilishaji, kupitia mikoa iliyopo nchini ili kupata takwimu sahihi za matendo ya udhalilishaji.

Akiwasilisha rasimu ya fomu ya ukusanyaji data Mkuu wa Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini bi Khadija Mohammed Abdallah amesema kuwa kesi nyingi zinazoripotiwa ni za kulawiti, shambulio la aibu pamoja na kubakwa.

Mkutano huo ambao ulikuwa una malengo ya uwasilishaji wa rasimu na nyenzo kwa ajili ya ukusanyaji na kupokea taarifa za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini.

MWISHO

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.