Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi, Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2023.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati tarehe 27 Januari, 2023 walisaini Mkataba wa makubaliano (Memorandum of Understanding) na Kampuni hiyo ya ENOC LLC kuhusu Ujenzi wa Kitovu cha Mafuta (Fuel Hub) hapa nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi pamoja na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi pamoja na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi pamoja na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.