Mkoa wa
Kusini Pemba
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema
uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi ni njia sahihi inbavyosaidia Viongozi
kutimiza vilivyo matarajio na matumani ya wananchi katika kukuza maendeleo ya nchi kuichumi na
kijamii.
Mhe. Othman
ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo huko Viwanja
vya Tibirinzi Chake Chake Pemba alipozungunza katika mkutano wa hadhara wa
chama hicho ikiwa ni muendelezo wa kutangaza ahadi za Chama hicho kwa wananchi.
Mhe Othman
amefahamisha kwamba nchi yoyotoe haiwezi kupiga hatua ya kimaendeleo iwapo
viongozi wake hawatoweka mbele suala la
masalahi ya wananchi sambamba na kuzingatia
udilifu katika kuwahudumia wananchi na shughuli za uendeshaji wa nchi na
kwamba chama cha ACT wazalendo
kinaswasilia kwa wananchi maono ya mabadiliko ya kimaendeleo katika kipindi cha
miaka kumi ijayo.
Amewataka
wananchi kuungana pamoja katika kuujenga Zanzibar mpya , yenye umoja na mamkala kamili itakauoweza kutumia
rasilimali zake mbali mbali ikwemo uwezo wa usarifu na upangaji wa kodi mbali
mbali katika kuongeza mapato ya wananchi na kukuza jitihada za kimaendeleo.
Mhe. Othman
amefahamisha kwamba katika uendeshaji wa nchi
kunahitajika viongozi kwa
wazalendo wenye kutumia maarifa na uwezo wao ipasavyo wa kuwatumikia wananchi kutimiza
malengo mbali mbali wanayojiwekea .
Amesema
kwamba hatua hiyo pia ni muhimu katika kujenga amani kweli nchini
inayotokana na kuwepo matumaini
makubwa ya imani kwa viongozi
katika kuleta mabadiliko yanayotokana na uwezo wa ndani wa rasilimali
zilizopo bila kuwepo vipingamizi vya namna yoyote.
Amefahamisha
wananchi ni vyema wakaunga mkono jitahada za viongozi wa ACT- Wazalendo kwa
kuwa viongozi wanaelekeza maono yao katika kupiga hatua za maendeleo kama
zilivyofanya nchi nyengene mbali mbali
ambazo mazingara yao ya kijiographia na uchumi yanafanana na Zanzibar.
Naye
Mwenyekiti wa Chama hicho Babu Juma Dunia Haji amewataka wananchi wa Zanzibar
kuungana ili kuendana na maono na mipango ya fikra za viongozi wa Chama hicho
za kuleta mabadiliko ya kisera na uwajiabikaji
utakaosaidia kiuchumi na na
maendeleo bora ya Zanzibar.
Amefahjamisha
kwamba viongozi waote wa chama hicho wanasimama
kutetea maslahi ya Zanzibar ikiwemo umoja haki na maridhiano ya kweli
ambayo ndio chachu ya kuleta na kudumisha Amani ya kweli katika nchi yoyote
duniani.
Naye Katibu
Mkuu wa Chama hicho Ado sahib Ado, amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka 2025 chama hicho kinahitaji kuwepo katiba Mpya, Mabadiliko katika sheria
ya Uchaguzi kwa kuwa ndio mamabo
yanayoweza kuleta haki.
Kwa upande
wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ismail Jussa Ladhu amewataka wananchi
wa Zanzibar kutokata tamaa na waendelee
kujenga mshikamano na umoja katika kujenga chama hicho ili juhudi za pamoja
zitumike kuweza kuleta maendeleo ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment