Katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Kwanza wa Rais Omar Dadi Shajak akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kuanzi April hadi june 2023 mbele ya wajumbe wa kamati ya kusimamia viongozi wakuu wa Kiatifa ya Baraza la Wawawakilishi wakati walipofanya ziara ya kiutendaji Ofisini hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Haroun Said Sleiman akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa kamati ya kusimamia viongozi wakuu wa Kiatifa ya Baraza la Wawakilishi wakati walipofanya ziara ofisini hapo.
Mwenyekiti kamati ya ya kusimamia viongozi wakuu wa Kiatifa ya Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wakati wa Ziara ya kamati hiyo kuangalia utendaji kazi katika Ofisi hiyo.
PICHA NA FAUZIA -MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Mussa Maelezo.
Kamati ya kusimamia Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la wawakilishi imeridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais kwa kipindi cha robo ya nne April- June 2023.
Akizungumza na watendaji wa Ofisi Hiyo hivi karibuni mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji kwa robo mwaka,Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia Viongozi Wakuu wa Kiatifa Machano Othman Said amesema Kamati itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ili kuhakikisha tatizo la uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya linamalizika Zanzibar.
"Waathirika zaidi wa Madawa ni vijana na watoto wetu ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo tukishirikiana tutashinda vita dhidi ya madawa ya kulevya". Alifahamisha Mwenyekiti huyo.
Ameeleza kuwa jukumu la kupambana na Madawa ya kulevya sio la mamlaka pekee hivyo ameishauri jamii kushirikiana katika kutokomeza dawa hizo.
Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Katibu Mkuu Ofisi hiyo Dk. Omar Dadi Shajak amesema katika kipindi cha robo ya nne April -June 2023 Ofisi imetekeleza jumla ya miradi mitano ikiwemo mradi wa ujenzi wa kituo cha tiba na marekebisho ya tabia ili kupunguza tatizo la madawa ya kulevya .
Hata hivyo amesema Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya imtoa elimu juu ya athari za Madawa hayo kwa wananchi , waalimu na Wananfunzi mbalimbali Unguja na Pemba .
Nao Wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza watendaji wa Ofisi hiyo kwa kuzingatia ilani ya chama cha mapinduzi 2020-2025, maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi,dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 , Malengo ya maendeleo endelevu ya dunia 2030 pamoja na maendeleo ya Ofisi ya makamo wa kwanza wa Rais katika utendaji wao.
No comments:
Post a Comment