Habari za Punde

Kongamano la Kimataifa la Masuala ya Uchumi wa Bahari lafanyika Mumbai, India

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mheshimiwa Suleiman Masoud Makame, wiki hii ya tarehe 16 hadi 20 Oktoba 2023 aliungana na viongozi wengine wa kimataifa kushiriki katika Kongamano Kuu la Kimataifa la Masuala ya Uchumi wa Bahari lililofanyika Mumbai, India. Kongamano hili la kimataifa liitwalo Global Maritime India Summit 2023, lilishirikisha mada mbali mbali zinazohusiana na Sekta za Utalii, Uvuvi, Usafiri na Usalama wa Bahari, Mafuta na Gesi na Diplomasia ya Uchumi wa Bahari.
Mheshimiwa Waziri Suleiman Masoud Makame alikuwa mmoja wapo wa watoa Mada hizo na alialikwa kuzungumzia masuala ya usafiri wa bahari na miundombinu ya bandari na pia kuwasilisha mada nyengine muhimu ya utalii wa bahari na fursa zilizopo za utalii na Uchumi wa Buluu.
Katika mchakato huo, Mheshimiwa Suleiman alisisitiza haja ya kuimarishwa kwa mashirikiano ya karibu kabisa baina ya India na Tanzania na hususan katika kupeleka mbele agenda ya Uchumi wa Buluu ya Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.