RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru Waumini wa dini ya
Kiislam wa Mkoa wa Kusini Unguja, kwa nia yao njema ya kumuombea dua na
kuliombea dua taifa.
Amesema, utamaduni wa kuiombea dua nchi
na viongozi lazima uendelezwe na udumishwe hasa wakati huu ambao dunia
imegubikwa na mabalaa mengi yenye athari mbaya.
Al hajj Dk. Mwinyi ameyasema hayo
kwenye dua maalum iliyoandaliwa na Wazee na viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja,
kwa kumuombea dua yeye na taifa kwa kipindi chote cha uongozi wake. Dua hiyo
imefanyika msikiti wa Ijumaa, Makunduchi Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini
Unguja.
Alisema, hakuna jambo jema kwa wakati
uliopo zaidi ya kumuomba Mwenyezi Mungu aiepushe nchi na mabala ya vita,
mabadiliko ya taiba nchi na mazingira ikiwemo upepo mkali na mafuriko.
Akizungumzia suala la amani, utulivu na
mshikamano wa nchi na watu wake, Al Hajj Dk. Mwinyi alisema amani na utulivu wa
nchi ndio kila kitu kwa mustakbali mwema wa maendeleo endelevu na ustawi wa
taifa na uchumi wake.
Akitolea mfano mataifa ya Urusi,
Ukraine, Sriya, Iraq na nchi nyngine duniani zilizogubikwa na vita pamoja na
mataifa yaliyoathiriwana ukame ikiwemo Pakistani, Al hajj Dk. Mwinyi alisema
dunia imekua kama Kijiji, inashuhudiwa mabalaa mengi ya vita na majanga ya
kimaumbile yanavyoiathiri, hali ilizusha taharuki na uchumi wa dunia
kutetereka, ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha na uchumi wa dunia.
Al hajj Dk. Mwinyi aliongeza hali hiyo pia
imeathiri sana mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania na Zanzibar kwa ujumla,
hivyo alilisitiza utamaduni wa kuendelea na kudumisha suala la kuiombea dua
nchi na viongozi wake.
“Tunawajibu wa kuendelea kumuomba
Mwenyezi Mungu atuepushe na mabalaa mbalimbali, mabalaa ya vita na matatizo ya
kimaumble, mabadiliko ya mazingira ikiwemo upepo mkali na mafuriko” aliomba Al
hajj Dk. Mwinyi.
Akizungumzia maendeleo makubwa
yaliyofikia na awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Al hajj Dk.
Mwinyi alieleza kuwa imeendelea kufanya mengi makubwa ikiwemo kufanikisha
miradi mingi ya maendelo na kuimarisha miundombinu ya mawasiliano zikiwemo
barabara za kisasa zenye viwango vya hali ya juu, ujenzi na uimarishwaji wa
huduma za elimu, afya, miradi mingi ya maji kwa kujengwa skuli na hospitali za
kisasa zenye hadhi za hali ya juu.
Pia, aliahidi kuendelea kupeleka miradi
mikubwa ya maendeleo mkoani humo na maeneo mengine ya nchi.
Akizungumza kwenye dua hiyo, Waziri
Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali
Suleiman aliwasihi wananchi wa Zanzibar kuendelea kumuombea dua Al hajj Dk.
Mwinyi kwa maendeleo makubwa anayoyafanya nchini.
Akitoa neno la shuqrani kwa niaba ya masheikh na wazee wa
Makunduchi, Shekh Muadhini Jongo ameshukuru Al hajj Dk. Mwinyi kwa kuridhia
kufika Makunduchi kujumuika nao kwenye dua hiyo pamoja na kuwashukuru Waislam
wote walioshirikiana kuifanikisha.
Dua hiyo, pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini
wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheik Saleh Omar Kaab pamoja na viongozi
wa Chama na Serikali.
Pia, Al hajj Dk. Mwinyi alizuru makaburi ya aliekua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Awamu ya nne, Marehemu Sheikh Iddrisa Abdul Wakili na
Kaburi la Sheikh Hassan bin Ameir, aliekua mwanazuoni mkubwa Zanzibar.
IDARA YA MAWASILIANO
IKULU, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment