Na Fauzia Mussa, Maelezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Wilaya ya kati Unguja Ndg.Said Hassan Shaaban amesema baraza la mji kati limepanga mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo.
Ameyasema hayo katika kikao cha madiwani wa wilaya hiyo
kilichofanyika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na ujenzi
wa vituo vya daladala ambapo tayari vituo kumi
vimeshajengwa na vipo katika hatua ya mwisho ili kuanza
kutumika.
Aidha ameeleza kuwa Baraza hilo limejipanga kuiendeleza
miradi ya masoko iliyojengwa katika Wilaya hiyo pamoja na
bustani zinazotarajiwa kutengenezwa katika maeneo ya
Hanyegwamchana na Tunguu.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa baraza la mji kati,
mkuu wa idara ya rasilimali watu, mipango, utawala na
mtumzaji kumbu kumbu Rehema Khamis Hassan amesema
watahakikisha kuwa wafanyakazi wa baraza hilo
wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kufikia malengo
yaliokusudiwa.
Aidha amesema watahakikisha ofisi ya baraza la mji kati
inatekeleza miradi yote ya kimkakati ambayo imewekwa
sambamba na uimarishaji wa miji katika robo ya mwaka
inayomalizia 2024_2025.
kikao hicho ni cha tatu Kufanyika katika Baraza la tano la
madiwani ndani ya Wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment