Habari za Punde

Serikali imedhamiria kumaliza Matatizo ya kiafya wanayokabiliana nayo Wananchi Wanaoishi katika Visiwa Vidogo vidogo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Boti Tatu za  Kusafirisha Wagonjwa “Ambulance Boat” uzinduzi huo uliyofanyika lkatika eneo la Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 19-2-2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kumaliza Matatizo ya kiafya wanayokabiliana nayo Wananchi Wanaoishi katika Visiwa Vidogo vidogo kwa  kufikishwa katika Matibabu  kwa wakati ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika ikiwemo vya akinamama na watoto.

Rais Dkt, Mwinyi ametoa tamko hilo baada ya kuzindua Boti za kubeba Wagonjwa wakati wa dharura hafla iliofanyika Verde Mtoni , Wilaya ya Mjini.

Amefahamisha kuwa Boti hizo ni sehemu ya uimarishaji wa huduma za dharura na mfumo wa wa Rufaa kwa Wagonjwa wanaotoka kwenye Visiwa wanaopewa Rufaa kutoka Vituo vya Afya kwenda Hospitali za Wilaya, Mkoa na Taifa.

Dkt,Mwinyinameiagiza Wizara ya Afya kuandaa Utaratibu mzuri wa matumizi ya Boti hizo ikiwemo matengenezo ya mara kwa mara iinapohitajika ili kuhakikisha zinafanya kazi  muda wote kufikia lengo lililokusudiwa.

Rais Dkt, Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali imeamua kuzipeleja Boti hizo katika maeneo yenye changamoto kubwa zaidi na kwengine  kutafanyiwa utaratibu wa Haraka baadae.

Aidha ametoa rai kwa Wananchi kutumia huduma hizo kwa  taratibu zilizowekwa na Wizara ya Afya na kuwatumia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kwa Dharura yoyote inapotokea ili waweze  kuwasaidia kwa haraka kupunguza madhara yanayoweza kuepukika.

Dkt, Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kusaidia gharama za  Ununuzi wa Boti Tano ambazo tatu tayari zimekamilika na mbili zitakamilika muda mfupi Ujao.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Meneja wa Benki ya Dunia Kanda ya Mashariki na  Kusini mwa Afrika Ernest Massiah amesema Boti hizo zitaweka utofauti baina ya Uhai na Kifo  na kuchochea dhamira ya Zanzibar kuwa kituo pekee Tiba na Matibabu  kinachotambulika  Kimataifa  na kuahidi kwa Benki ya Dunia kuendelea Kuisaidia Zanzibar.

Naye Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui  amewahakikishia Wananchi wanaoishi katika  Visiwa  huduma za Uhakika zitakazoanza hivi karibuni na kuwa tayari  Kuzitumia huduma hizo hususan akina Mama na watoto.

Boti hizo zimegharimu takribani Shilingi Bilioni 2 na zimetengenezwa na Kampuni ya QIRO GROUP LIMITED.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.