Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kikao cha Bajeti ambapo kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Na Sabiha Khamis - Maelezo Zanzibar 05.05.2025
Mkutano wa 19 wa Baraza la 10 la Wawakilishi unatarajiwa kuanza Mei 07 na kumalizika Juni 20 mwaka huu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Katibu wa Baraza hilo, Raya Issa Mselem katika ukumbi wa Mikutano Baraza hilo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar amesema mkutano huo unahusisha maswala ya bajeti kwa ujumla.
Amesema pia mkutano huo utahusisha na kuendesha shughuli mbalimbali za Baraza ikiwemo maswali na majibu ambapo ofisi ya Baraza la Wawakilishi limepokea na kuratibu maswala 311 kwa ajili ya mkutano huo.
Ameeleza kuwa shughuli nyengine zitazofanyika ni pamoja na majadiliano na kupitisha bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2025 – 2026 na Miswada miwili ya sheria.
Ameitaja miswada yenyewe ni mswada wa Sheria ya fedha ya mwaka na mswada wa kisheria ya matumizi ya mwaka 2025 – 2026.
Aidha Katibu huyo amefahamisha baada ya kupitisha bajeti zote za serikali kwa Baraza la 10 la Wawakilishi la Zanzibar litavunjwa kutokana na kufikia muda wa miaka mitano wa maisha ya Bazara hilo kama katiba inavyoeleza.
Baraza hilo linatarajiwa kuvunjwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kumalizik kwa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji akifafanua jambo wakati akijibu baadhi ya Maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kikao cha Bajeti ambapo kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Jesse Mikofu akiuliza maswali katika Mkutano wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kikao cha Bajeti ambacho kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Nipashe Rahma Suleiman akiuliza maswali katika Mkutano wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kikao cha Bajeti ambacho kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waiohudhuria katika Mkutano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem kuzungumzia Kikao cha Bajeti ambacho kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Afisa Habari wa Habari Maelezo Sabiha Khamis akifuatilia Mkutano wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kikao cha Bajeti ambacho kitaanza Tarehe 7 Mey na kinatarajiwa Kumalizika 20 June,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.05/05/2025.
No comments:
Post a Comment