Habari za Punde

WAZAZI, WALEZI JIPANGENI KUWAPATIA ELIMU WATOTO

Na Madina Issa

WAZAZI na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao kwa lengo la kuwapatia elimu kwani elimu ndio inayomfanya mtoto awe na maadili mazuri na kuweza kutojiingiza katika makundi maovu.

Meneja wa hoteli ya Mszon, Kapara Khamis Kapara aliyasema hayo alipokuwa katika mahafali ya kuwakabidhi vyeti wanafunzi waliohitimu mafunzo ya awali wa skuli ya MT Joseph's iliopo shangani mjini
yaliyofanyika katika skuli ya Haile Selassie.


Alisema wazazi na walezi endapo watakaa pamoja, wataweza kuchangia kuwapatia elimu na kuwa msingi wa kuwafumbua macho na kuweza kujitoa hata katika makundi maovu ambayo yanaweza kuharibu maendeleo yao.

Kapara alisema kuwa amefarajika kuwaona walimu, wazazi wapo pamoja na watoto wao kwa kuweza kushirikiana kwa kuwapatia elimu iliyobora watoto wao kwani inaweza kuwasaidia baadae katika maisha yao.

Mapema mwanafunzi Tamila Elias Mwamwana akisoma risala, aliwapongeza walimu wao kwa kuwaonesha mwangaza ambao sasa wameweza kufaidika nao.

Hata hivyo, alisema kuwa mbali na wazuri waliyokuwa nao lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa vitendea kazi kama computa kwa ajili ya kufanyia mazoezi ya vitendo pamoja na
kufanyia mitihani yao.

Tamila alimuomba Meneja huyo awapatia mabasi kwa ajili ya kuwarahisishia kuwahi skuli kwani hivi sasa wamekuwa hawana usafiri wa uhakika wa kwendea skuli hivyo inawasababishia hata kuchelewa kuwanza
masomo yao mapema.

Meneja huyo aliahidi kushirikiana na wazazi, walezi pamoja na walimu na kuwaahidi kuwapelekea Komputa mbili kwa lengo la kuwasaidia katika kazi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.