Habari za Punde

Jamuhuri Yaongoza ligi kuu ya Zanzibar

Na Haji Nassor, Pemba

TIMU ya soka ya Jamhuri, imeshika usukani wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya juzi kuwafunga wakongwe wenzao Chipukizi bao 1-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa uwanja wa Gombani.

Bao hilo pekee liliopachikwa nyavuni na mchezji machachari Ali Othman Mmanga katika dakika ya 25 aliyeunganisha vyema mpira wa krosi uliochongwa na Bakari Khamis.


Kufuatia ushindi huo, Jamhuri iliyoiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu na kutolewa na Hwange FC ya Zimbabwe, imefikisha pointi 28 ikifuatiwa na Super Falcon yenye pointi 26.
Miembeni United na KMKM zinashika nafasi ya tatu kwa pamoja zote zikiwa zimefikisha pointi 25. lakini zikipitana na kwa magoli ya kufunga na kufungwa.

Wakati huohuo, klabu ya Cossovo ya Chumbageni Wambaa, imefanikiwa kusonga mbele hatua ya nane bora, kwenye ligi daraja la pili Wilaya ya Mkoani, baada ya kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 19.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ushndi mnono katika mechi mbili za mwishoni, ambapo vijana hao waliifunga Datisho magoli 4-1, kabla ya kuinyanyasa Machabo kwa kipigo cha mabao 8-0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.