Mbuge wa Jimbo la Makunduchi ambaye pia ni Waziri wa nchi Afisi ya Makamo wa Rais anayeshughulikia Muungano akijitayarisha kukata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji kijijini Mzuri Kaja, Makunduchi. Mradi huu uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 10 umefadhiliwa kwa mashirikiano baina ya Jumuiya ya Maendeleo ya Watu wa Mzuri Kaja (MKDS) www.mzuri-kaja.or.tz pamoja na Jumuiya itwayo GETWELL Tanzania kutoka Sweden. Kisima kilichochimbwa kimewekewa tangi la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita elfu 10 kwa mpigo. Mradi huu ni endelevu kwani wananchi huchangia kwa kununua maji kwa bei ya ndoo 5 kwa shillingi 100. Wanakijiji wameamua kuunda kamati ya maji ambayo tangu kuanza kutumika maji mienzi 5 iliyopita imejikusanyia zaidi ya shilingi milioni moja. Lengo la kamati hii ya maji kujenga visima vyengine kijijini hapo, pamoja na kufanya matengenezo matogo madogo yatakayotokea. Mhe. Waziri amewataka wanakijiji kuutunza mradi huu kwa maendeleo yao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango
Amefanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa IEA
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana
na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa International Energy A...
11 minutes ago
No comments:
Post a Comment