Na Fatina Mathias, Dodoma
Serekali imesema itamaliza
kulipa madeni ya watumishi wa umma kiasi cha shilingi bilioni nane mwezi
Novemba na Disemba mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani,
alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salum, aliyetaka kujua kwa nini serikali
inakuwa na malimbikizo ya watumishi ya muda mrefu.
Alisema mpaka sasa serikali
inadaiwa shilingi bilioni 8 kwa upande wa watumishi wa umma na itahakikisha
inalipa kuanzia Novemba na Disemba.
Alibainisha kwa watumishi wa mambo
ya ndani ya nchi wanadai kiasi cha shilingi milioni 800.
Alisema wakati mwingine hali ya
malimbikizo hayo yanatokana na baadhi ya watumishi wapya kuchelewa kupitia
kazini pindi wanapoajiriwa.
“Kwa utaratibu uliopo hivi
sasa,mtumishi anapoajiriwa na kuwahi kuripoti kazini,mwisho wa mwezi anapata
mshahara wake isipokuwa kwa wake wanaochelewa kuripoti,”alisema.
Alisema sasa mtumishi
anayeajiriwa na kuripoti kazini kuanzia tarehe moja hadi 10, mwisho wa mwezi
anapata mshahara wake kama kawaida, na wanaoripoti baada ya tarehe 10, wanaweza
kukosa mshahara wa mwezi husika.
No comments:
Post a Comment