Habari za Punde

Mafunzo ya haki za binadamu kwa vyama vya wafanyakazi ZATU

 AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akitoa maelezo mafupi ya mafunzo ya haki za binadamu kwa vyama vya wafanyakazi ZATU yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria afisini mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 WANACHAMA wa chama cha waalimu ZATU kanda ya Pemba, wakisikiliza mada kadhaa zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mafunzo ya haki za binadamu kwa wanachama hao, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akielezea namna kituo hicho kinavyofanyakazi kwa kuwapa wananchi elimu ya sheria, kwenye mafunzo ya haki za binadamu kwa wanachama wa chama cha waalimu ZATU kanda ya Pemba, kulia ni Afisa Mipango wa ZLSC Khalfan Amour Mohamed na kushoto ni Katibu wa ZATU Juma Khatib Faki, (Picha na Haji Nassor, Pemba ).
 KATIBU wa Chama cha Waalimu Zanzibar kanda ya Pemba Juma Khatin Faki, akifungua mafunzo ya haki za binadamu kwa wanachama wa chama hicho, mafunzo hayo yalifanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MTOA mada kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Siti Habib Mohamed akiwasilisha mada ya sheria mahusiano kazini kwenye mafunzo ya haki za binadamu kwa wanachama wa chama cha waalimu ZATU, yaliofanyika ZLSC mjini Chakechake (Picha na Haji Nassor, Pemba). 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.