Habari za Punde

JUMUIYA YA JUKWAUPE YATOA MSAADA KWA WAZEE WASIOJIWEZA WA VIJIJI VYA FUMBA NA BWELEO

Wafanyakazi wa Jumuiya ya kuwasaidia na  kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE)  wakiwa katika Kijiji cha Fumba kwa ajili ya kutoa msaada  kwa wazee wasiojiweza wa kijiji hicho
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kuwasaidia  na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE)  Khamis  Mussa Juma akimkabidhi msaada Mohammed Hassan Shoka.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kuwasaidia  na kuwaenzi wazee wasiojiweza Khamis  Mussa Juma akimkabidhi msaada Fatma Shani Ameir.
 Msaidizi Fedha wa  Jumuiya ya kuwasaidia  na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE)  Ramadhan Ali Juma akimkabidhi msaada Maryam Mataka Mohammed.
 Msaidizi Fedha wa  Jumuiya ya kuwasaidia  na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE)  Ramadhan Ali Juma akimkabidhi msaada Amana Kombo Khamis wa Bweleo.
Mjumbe wa  Jumuiya  ya kuwasaidia  na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE)  akimkabidhi msaada Mwashamba Gharib Mkame katika hafla iliyofanyika Fumba.
                        Picha Na Miza Othman Maelezo- Zanzibar.
Na Kijakazi Abdalla         Maelezo               19/10/2018
JAMII imetakiwa kuwatunza  na kuwaenzi  wazee wasiojiweza ili  wajione kuwa ni sehemu ya jamii inayohitaji matunzo na kuondokana na upweke baada ya mchango mkubwa waliotoa wakati wa ujana wao.  
Akizungumza katika hafla ya kuwafariji wazee wasiojiweza katika vijiji vya Fumba na Bweleo, Katibu wa Jumuiya ya Kuwasaidia Wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) Khamis Mussa alisema wazee wanayokila sababu ya kusaidiwa kutokana na juhudi zao katika maendeleo ya Taifa .
Alikumbusha kuwa malipo yanayotokana na kuwasaidia wazee ni makubwa mbele ya Allah na amewashauri wananchi kuwa karibu nao ili kujenga upendo na kujihisi kuwa bado wanathamani ndani ya jamii wanazoishi.
Alisema kuwa lengo la kuanzisha jumuiya JUKWAUPE ni kutafuta misaada kutoka kwa wasamaria wema na kuifikisha kwa wazee hasa huduma muhimu za  chakula, nguo na huduma ya afya.
Alieleza kuwa Jumuiya hiyo imejikita zaidi kusaidia wazee wasiojiweza wenye umri kuanzia miaka 80 wanaoishi vijijini ambao mara nyingi wanashindwa kukidhi mahitaji yao ya lazima katika maisha.
Sheha wa Shehiya ya Bweleo Mataka Ame Mataka aliishukuru jumuiya hiyo kwa msaada walioutoa na kuzitaka jumuiya nyengine kuiga mfano kama huo wa kuwasaida wazee kwani kutoa ni moyo .
Aidha alizitaka Jumuiya nyengine zenye nia ya kutoa msaada hasa wa chakula na dawa kutoa taarifa katika taasisi husika kuhakikisha usalama wa msaada huo na kuepuka usumbufu wanapofika vijijini.
“Kuna baadhi ya Jumuiya huenda katika vijiji kwa lengo la kutoa msaada lakini wanashindwa kufuata taratibu na hatimae kupata usumbufu usiowalazima,’’ alikumbusha Sheha Mataka.
Wazee waliopatiwa msaada huo wameishukuru JUKWAUPE na kuwataka kuendelea kuwasaidia kila hali itakaporuhusu ili wajihisi kuwa bado wanajaliwa na kuthaminiwa.
 IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.