Habari za Punde

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe.Kanyasu Awahimiza Wafanyabiashara za Utalii Kuwekeza Mikoa ya Kusini.

Naibu Waziri   wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constanine Kanyasu (wa pili kulia) akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Richard Kasesela (wa kwanza kulia)  wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kanda ya Mikoa ya Nyanda za juu Kusini wa Idara ya Utalii, Tully Kulangwa wakati  wakitembelea mabanda kabla ya Naibu Waziri huyo  kufungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa
Naibu Waziri   wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constanine Kanyasu akipata maelezo kutoka kwa Afisa Misitu wa Shamba la miti la Sao Hill kuhusu asali inayozalishwa kwenye shamba hilo kutoka kwa Idd Amosi wakati  akitembelea mabanda kabla ya kufungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Naibu Waziri   wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constanine Kanyasu (wa pili kulia) akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Richard Kasesela (wa kwanza kulia)  wakiangalia mafuta kwa ajili ya chakula yaliyotengenezwa kwa kutumia parachichi na Mjasiliamali Ayubu Sanga wakati  wakitembelea mabanda kabla ya  Naibu Waziri huyo  kufungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa
Viongozi mbalimbali wakiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakiimba wimbo wa taifa kabla ya  kufungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Naibu Waziri   wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constanine Kanyasu akizungumza na wananchi wakati akifungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Richard Kasesera akizungumza na wananchi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akifungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakatai wa ufunguzi wa m Maonesho ya tatu ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Baadhi ya kikundi cha burudani cha kabila la wamasai kikitumbuiza mara baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akifungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa

Na.Lusungu Helela - WMU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constanine Kanyasu  ametoa wito kwa wafanyabiashara za utalii nchini kuwekeza katika mikoa ya Nyanda za juu  Kusini ambayo ina vivutio vingi vya utalii.
Pia, Amesema kuwa wizara yake itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hao  kwa kupunguza masharti kwa kampuni binafsi za utalii hasa za wazawa ili kuongeza tija katika biashara ya utalii nchini.
Amebainishwa hayo  wakati Naibu Waziri  huyo akifungua Maonesho ya tatu ya  Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa yenye kauli mbiu isemayo’’ Karibu Kusini Ufurahie Utalii Wetu’’
Akitaja mikoa hiyo ya Nyanda ya juu kusini kuwa ni  Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi, Mhe. Kanyasu amesema kuwa mikoa hiyo  imejaliwa kuwa na idadi kubwa ya vivutio vya kihistoria, kiutamaduni na kiikolojia vinavyofanya upekee wa mikoa hiyo  katika sekta ya utalii hapa nchini na ulimwenguni.
Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu amewataka wafanyabishara hao  waanze kuwekeza miundombinu ya utalii  kama vile kujenga hoteli pamoja na kufungua kampuni za utalii katika ukanda huo badala ya kuendelea kuwekeza zaidi katika mikoa ya Kaskazini.
Katika hatua nyingine,Mhe,Kanyasu ameiagiza  Mikoa yote nchini  kutenga bajeti  kwa ajili ya kuendeleza vivutio vya utalii ikiwa pamoja na  kuvitunza kuvitangaza vivutio hivyo.
 Aidha, Mhe, Kanyasu amewasihi Wakuu wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kushiriki kikamilifu  katika maonesho hayo kwa  pamoja na kuwa na vikao vya mara kwa mara na wadau wa utalii katika Mikoa hiyo ili  kuimarisha maendeleo ya sekta ya utalii katika mikoa hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bw. Richard Kasesela amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) imeitenga mikoa hiyo kwa vile katika maonesho ya Utalii ya Nje za nchi, TTB imekuwa haivitangazi vivutio vilivyoko Nyanda za Juu Kusini.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amemuomba Naibu Waziri Mhe. Kanyasu aiagize TTB itoe kipaumbele kwa kutangaza vivutio vya mikoa hiyo katika maonesho ya  ndani na nje ya nchi ili vivutio wa mikoa hiyo viweze kujulikana  kama vivutio vya  mikoa ya kaskazini.
Maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yalizinduliwa  mwaka 2016 yakiwa yamelenga kuchochea maendeleo ya utalii kwa Mikoa ya Kusini kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.