Habari za Punde

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe.Balozi Amina Salim Ali Awasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021.


HOTUBA YA WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021
MHESHIMIWA:  BALOZI AMINA SALUM ALI (MBM)


i
                                       HOTUBA YA WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA
MHESHIMIWA BALOZI AMINA SALUM ALI,
KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021:

1       UTANGULIZI :

1.       Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba
Baraza lako Tukufu sasa likae kama Kamati ya Mapato na Matumizi kwa madhumuni ya kupokea, kuzingatia, kujadili na hatimae kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kazi za kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

2.       Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwezesha kufika katika ukumbi huu hii leo tukiwa wazima na afya njema na pia kutuwezesha kuendelea kutekeleza majukumu ya kujenga nchi yetu kwa usalama, amani na ufanisi mkubwa katika kipindi chote cha miaka 10 ya awamu ya saba ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 

3.       Mheshimiwa Spika, Naomba kuchukua fursa hii adhimu kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi kwa kusimamia kwa umakini mkubwa utekelezaji
wa mipango ya kitaifa na kimataifa, hususan uendelezaji wa Sekta ya Biashara na Viwanda, Dira ya Maendeleo 2020, pamoja na utekelezaji wa malengo ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010 – 2020.

4.       Mheshimiwa Spika, Pia nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa jitihada zake za dhati anazozichukua za kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kuwatumikia wananchi wa Zanzibar. Vile vile kwa kutupatia miongozo, maelekezo na maagizo yake katika maendeleo ya nchi yetu.

5.       Mheshimiwa Spika, Nathubutu kutamka kwamba katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Saba, mafanikio makubwa yamepatikana katika Sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Biashara na Viwanda. Aidha, kama nitakavyoeleza katika Hotuba yangu huko mbele, Serikali ya Awamu ya Saba imeweka msingi imara wa maendeleo endelevu ya Sekta za Biashara na Viwanda na nchi yetu kwa ujumla.
Hivyo, sina budi kumshukuru kwa namna ya kipekee kabisa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa imani yake kubwa kwangu kwa kunikabidhi dhamana ya kuiongoza Wizara ya Biashara na Viwanda ambayo ndio sekta kiongozi katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii katika Taifa letu.
6.       Mheshimiwa Spika, Nina hakika kuwa nimetumia juhudi na uwezo wangu wote alionipa Mwenyezi Mungu kutekeleza kazi na dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na ni matumaini yangu kuwa mafanikio tuliyofikia yataendelezwa kwa nguvu na msukumo wa ziada katika uongozi wa Serikali ya Awamu inayokuja.

7.       Mheshimiwa Spika, Naomba kuchukua fursa hii pia kukushukuru wewe binafsi pamoja na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Baraza bila kuwasahau wajumbe wa Baraza lako tukufu kwa mashirikiano makubwa na michango na ushauri mliotupatia kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Wizara, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na pia kwa ushauri na maelekezo yenu kuhusiana na utekelezaji wa malengo ya Wizara hii kwa mwaka ujao wa 2020/2021.

8.       Mheshimiwa Spika, Naomba kuchukua fursa hii kumpa pole za dhati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kukabiliana na janga la Ugonjwa wa COVID19 unaosababishwa na Virusi vya KORONA. Aidha, nawapa pole viongozi na Wananchi wote kwa ujumla kwa kuathirika kutokana na ugonjwa huu thakili. Salamu maalum za rambi rambi ziwaendee Wananchi wote waliopoteza ndugu zao na wale waliopoteza ajira kutokana na janga hili ambalo limeathiri sana Sekta mbali mbali za Kiuchumi na Kijamii.

9.       Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara na Viwanda katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa maradhi
ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya CORONA (COVID – 19), iliamua kufanya tathmini juu ya upatikanaji wa vifaa kinga vya maradhi hayo. Matokeo ya tathmini hiyo imeonesha kutokuridhishwa kwa vifaa hivyo na upandishwaji wa bei na vyengine havikidhi viwango au havifai kabisa.
10.    Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali (CGCLA) iliandaa na kutoa mafunzo ya kutengeneza vifaa kinga kwa wajasiriamali 25 pamoja na wahitimu wa vyuo 3 ambao wameshirikiana na wajasiriamali kuzalisha vitakasa mikono (sanitizer). Kwa upande wa barakoa (mask), Wizara imeshirikiana na kiwanda cha Serikali kilichopo Amani (ZQTL) kwa kukipatia aina (sample) na malighafi na wameweza kutengeneza. Lengo ni vifaa hivi viweze kupatikana kwa uhakika na kwa bei nafuu na kila mwananchi amudu kuvitumia.
11.    Mheshimiwa Spika, Bila shaka ugonjwa huu utakuwa na athari kubwa kwenye pato la mtu mmoja mmoja na kupunguza kasi ya ukuaji wa pato la Taifa. Hata hivyo, “Wahenga wanasema mwisho wa dhiki ni faraja” naamini tutavuka katika kipindi hiki kigumu tukiwa washindi kama tulivyovuka majanga mengine yaliyotokea miaka ya nyuma kama Kipindupindu, Ukimwi (HIV) na Malaria. Tumuamini Mwenyezi Mungu na tuongeze juhudi za kupambana na Ugonjwa wa COVID-19, bila ya shaka kwa kufuata masharti ya Wataalamu wa Afya na maelezo yanayotolewa na Serikali ugonjwa huu tutaushinda.

12.    Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya bajeti hii yamepitia katika hatua na ngazi mbali mbali za awali ikiwemo Kamati ya Uongozi ya Wizara na Kamati ya Kudumu ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi. Naomba kuchukua fursa hii kuishukuru sana Kamati hii inayoongozwa na Mheshimiwa Mwinyihaji Makame Mwadini, Mwakilishi wa Jimbo la Dimani kwa kuchambua mapendekezo ya awali ya bajeti hii na hatimae kuridhia kuwasilishwa mbele ya Baraza lako Tukufu kwa kujadiliwa na kuidhinishwa. 

13.    Mheshimiwa Spika, Aidha, shukurani zangu za pekee zimwendee Naibu Waziri wa Wizara hii Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh kwa mashirikiano yake makubwa anayonipatia katika kuhakikisha malengo ya Wizara yanafikiwa. Pia nawashukuru kwa dhati ndugu Juma Hassan Reli, Katibu Mkuu na ndugu Khadija Khamis Rajab, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hii, Wakurugenzi na viongozi wote wa Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wafanyakazi wote wa Wizara kwa juhudi zao kubwa za kuchapa kazi pamoja na mashirikiano makubwa wanayonipatia yaliyosaidia katika utekelezaji mzuri wa majukumu yangu.

14.    Mheshimiwa Spika, Matayarisho ya  bajeti hii yamezingatia miongozo mbalimbali iliyowekwa na Serikali ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020, Mpango wa Ukuzaji Uchumi na Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA III), Ilani ya CCM ya mwaka 2010 -2020, Sera za Biashara na Viwanda, maagizo yanayotolewa na viongozi wakuu wa
nchi pamoja na Ukomo wa Rasilimali Fedha uliopangiwa kwa Wizara.

15.    Mheshimiwa Spika, Pamoja na mazingatio ya hapo juu, utayarishaji wa mapendekezo haya ulizingatia pia matukio mbali mbali yaliyojitokeza ulimwenguni ambayo yamekuwa na athari za moja kwa moja katika mwenendo wa biashara, viwanda na uchumi duniani. Matukio hayo ni kama vile janga la Dunia lililojitokeza hivi karibuni la maradhi ya COVID–19 yanayosabishwa na virusi vya KORONA, kushuka kwa bei ya mafuta Duniani, kupungua kwa mwenendo wa uwekezaji duniani, kuathirika kwa mwenendo wa biashara na fedha pamoja na masuala ya kisiasa katika baadhi ya maeneo ya Dunia.

16.    Mheshimiwa Spika, Katika hotuba yangu hii, nitaanza kwa kufanya mapitio ya jumla kuhusu mwenendo wa biashara na hali ya viwanda, utekelezaji wa malengo ya bajeti ya Wizara kwa mwaka 2019/2020, na hatimae nitawasilisha mapendekezo ya bajeti kwa programu za Wizara kwa mwaka ujao 2020/2021.

2       MWENENDO WA BIASHARA :

17.    Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha awamu ya Saba, sekta ya Biashara imepata mafanikio makubwa kutokana na juhudi za Serikali za kuimarisha mazingira mazuri ya biashara na kurahisisha ufanyaji wa biashara hapa Zanzibar. Juhudi hizo zimepelekea kupitisha sheria mbali mbali, kuanzisha taasisi na kuziimarisha baadhi ya taasisi nyengine.

18.    Mheshimiwa Spika, Serikali katika juhudi zake za kulinda afya na usalama kwa watumiaji wa bidhaa, huduma na kuhifadhi mazingira nchini, ilitunga Sheria

Namba 1 ya mwaka 2011 ya Viwango, Zanzibar.                                               
Sheria hii ilianzisha Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) yenye malengo ya kuweka viwango na kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa au kuingizwa nchini kutoka nje ya nchi. Mpaka sasa ZBS imeanzisha maabara 3 (Kemikali, Vifaa vya umeme na Chakula) zinazofanya kazi, ujenzi wa Ofisi na maabara za ziada unaendelea katika eneo la Maruhubi.

19.    Mheshimiwa Spika, Serikali katika lengo la kurahisisha na kuendeleza Biashara Zanzibar imetunga Sheria Namba 13 ya Mwaka 2012, inayosimamiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA). Taasisi hii imepewa jukumu la kufanya usajili wa Biashara na Mali, ikijumuisha usajili wa taasisi za Biashara, Mali za Ubunifu pamoja na Usajili wa Nyaraka mbali mbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaoishi au wanaofanya shughuli zao Zanzibar. Tangu kuanzishwa BPRA, imerahisisha masuala ya usajili kwa kufanya marekebisho na mageuzi ya mifumo ya usajili wa Biashara na mali kwa kuandaa mifumo mipya ya usajili kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

20.    Mheshimiwa Spika, Katika kurahisisha na kuendeleza Biashara, Serikali imetunga Sheria ya Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara ya mwaka 2013 (The Business Licensing Regulatory Act No. 13 of 20I3). Lengo kuu la sheria hiyo ni kuondosha changamoto zote zinazoukabili mfumo wa utoaji leseni za Biashara uliokuwa ukiendelea kutumika. Sheria hiyo imeanzisha Baraza la Kusimamia Mageuzi ya Mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara (BLRC) ili kuweza kusimamia mageuzi kwa taasisi zinazotoa leseni. Tangu kuanzishwa kwa BLRC, hatua za upatikanaji wa leseni zimepungua sana, malipo ya leseni kufanyika kupitia benki na taarifa za leseni zinapatikana wa njia ya kielektoniki.
21.    Mheshimiwa Spika, Serikali katika kuhakikisha jukwaa la majadiliano ya Biashara baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yanatekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu imetunga Sheria Namba 10 ya mwaka 2017 inayosimamiwa na  Baraza la Taifa la Biashara (ZNBC). Madhumuni ya majadiliano haya ni kuwashirikisha sekta binafsi katika maendeleo ya nchi pamoja na kutatua kero mbalimbali za wafanyabiashara.
22.    Mheshimiwa Spika, Katika kusimamia ushindani halali wa kibiashara na kumlinda Mtumiaji, Serikali imetunga Sheria Namba 5 ya mwaka 2018 inayosimamiwa na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji (ZFCC). Taasisi hii ina lengo la kuhakikisha kuwa inaimarisha na kushajihisha ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji wa bidhaa na huduma Zanzibar.

23.    Mheshimiwa Spika, Katika kuendeleza Wajasiriamali wadogo wadogo, wadogo na wa kati Serikali imetunga Sheria Namba 2 ya mwaka 2018(Micro, Small and Medium Enterprises Act) inayosimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo vidogo, Vidogo na vya kati (SMIDA). Madhumuni ya Wakala ni kuwaendeleza na kuimarisha sekta ya uzalishaji viwanda kwa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kuleta tija na manufaa kwa Taifa. Tangu kuanzishwa kwa Wakala changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa Wajasiriamali imepungua pamoja na kuimarika kwa uzalishaji wa bidhaa wanazozalisha na kukidhi soko linalohitajika.

24.    Mheshimiwa Spika, Katika kuwatafutia masoko wajasiriamali wetu pamoja na kuhamasisha uzalishaji nchini, Wizara imekuwa ikiandaa matamasha ya biashara pamoja na kuratibu ushiriki wa wajasiriamali katika maonesho mbali mbali nchini, kikanda na kimataifa. Mheshimiwa Spika haya yote ni mafanikio katika sekta ya biashara yaliyopatikana katika awamu ya saba.

2.1    Hali ya Uchumi na Biashara Duniani :

25.    Mheshimiwa Spika, Katika hotuba yangu ya bajeti ya mwaka 2019/2020, nililiarifu Baraza lako Tukufu juu ya kuyumba kwa mwenendo wa uchumi na biashara duniani na jinsi mwenendo huo ulivyoathiri biashara kwa nchi mbali mbali ikiwemo Zanzibar. Naomba kuliarifu Baraza
lako Tukufu kuwa hali ya uchumi na biashara duniani bado haijatengemaa na inaendelea kutishia kasi ya ukuaji biashara Duniani na kuathiri mchango wa sekta hii katika uchumi wa dunia  (World Merchandise Trade Percentage of GDP) ambao unatarajiwa kupungua kwa asilimia 2.6 mwaka 2019 kutoka asilimia 3.0 mwaka 2018. Vile vile, kutokana na kulipuka kwa maradhi ya COVID19 yanayosababishwa na virusi vya KORONA ambayo yameikumba Dunia nzima tunatarajia kuendelea kushuka zaidi kwa mchango wa sekta ya biashara kwa mwaka huu wa 2020. Mchoro namba 1 unaonesha asilimia ya mchango wa biashara katika uchumi wa dunia.

Mchoro Namba 1:
Mchango wa Sekta ya Biashara katika Uchumi wa
Dunia 2016-2019


Chanzo: Shirika la Biashara la Dunia-WTO, 2020

26.                                       Mheshimiwa Spika, Usafirishaji wa bidhaa duniani kwa kipindi cha mwaka 2018 ulifikia USD 19.48 trilioni, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 10 ikilinganishwa na usafirishaji uliofanyika mwaka 2017. Katika kipindi cha mwaka 2019 uagiziaji kwa nchi za Marekani ya Kaskazini umeonesha kupungua kwa kasi ndogo wakati nchi za Marekani ya Kusini, Ulaya na Asia imeonesha kupungua kwa kasi kubwa. Hata hivyo kwa nchi nyengine zimeendelea kuonesha ongezeko la uagiziaji kutoka asilimia 1.9 mpaka asilimia 4.9 kwa mwaka 2019.

 Mheshimiwa Spika, Mwenendo huo wa usafirishaji na uagiziaji wa bidhaa duniani ni kwa mujibu wa taarifa ya makisio ya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kwa kipindi cha mwaka 2019.
2.2  
Hali ya Biashara Zanzibar
Usafirishaji na Uagiziaji wa Bidhaa:

27.                                       Mheshimiwa Spika, Hali ya biashara kwa ujumla imeonesha kuimarika kwa mwaka 2019, ambapo Zanzibar imefanya biashara yenye thamani ya Shilingi bilioni 478.52 ikilinganishwa na biashara ya Shilingi bilioni 394.04 mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 21.4. Biashara hiyo ilikuwa ni usafirishaji wa bidhaa kwenda nje ya Zanzibar na uagiziaji wa bidhaa kuja Zanzibar. Bidhaa ambazo Zanzibar ilisafirisha nchi za nje ni pamoja na karafuu, mwani, dagaa na majongoo ya pwani.


28.                                       Spika, Katika kipindi cha mwaka 2019,
Zanzibar ilisafirisha nje bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 131.65. Kiwango hicho cha usafirishaji ni sawa na ongezeko la asilimia 126.2 kwa kulinganisha na usafirishaji wa bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 58.19uliofanyika kipindi cha mwaka 2018. Katika usafirishaji huo, zao la karafuu lilikuwa na thamani ya Shilingi bilioni 19.85 sawa na asilimia 27.7 ya usafirishaji wote. Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa usafirishaji wa tani za karafuu katika kipindi cha mwaka huu ukilinganisha na mwaka 2018. Mnunuzi mkubwa wa karafuu za Zanzibar ni nchi ya India ikifuatiwa na Singapore.
29.                                       Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa uagiziaji bidhaa, nchi yetu iliagiza bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 346.88 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na uagiziaji wa Shilingi bilioni 335.84 mwaka 2018. Bidhaa ambazo Zanzibar imeagiza kutoka nchi za nje ni pamoja na vyombo vya usafiri, bidhaa za elektroniki, nguo na chakula ikiwemo mchele, sukari na unga wa ngano. Mwenendo wa biashara umeonesha kuimarika kwa urari wa biashara kwa kupunguza nakisi yake kutoka Shilingi milioni 277,660.6 hadi Shilingi milioni 215,231.1 kwa mwaka 2019 Mchoro Namba 2 hapa chini unatoa ufafanuzi zaidi.
Mchoro Namba 2:
Mwenendo wa Biashara Zanzibar (2010 – 2019)
2.3   Biashara Baina ya Zanzibar na Tanzania Bara (InterState Trade Balance):


30.              
  Mheshimiwa Spika, Biashara baina ya Zanzibar na Tanzania Bara inahusisha utoaji wa bidhaa kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara na uingizaji wa bidhaa kutoka Tanzania Bara kuja Zanzibar.  Biashara hiyo inahusisha bidhaa za vyakula, vifaa vya elektroniki, magari, madawa na vinywaji. Kwa miaka ya hivi karibuni, biashara kutoka Zanzibar kwenda Bara imeendelea kupungua na hivyo kusababisha urari mkubwa wa biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Hali hii ilitokana na vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru hasa vibali vya ruhusa ya kuingiza bidhaa na masuala ya usajili wa bidhaa.

31.          Spika, Kwa kipindi cha mwaka 2019, Zanzibar ilipeleka bidhaa Tanzania Bara zenye thamani ya Shilingi bilioni 21.56, ikilinganishwa na bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 24.29 zilizopelekwa mwaka 2018. Aidha, Zanzibar iliagizia kutoka Tanzania Bara bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 260.67 ikilinganishwa na uagiziaji wa bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 269.67 mwaka 2018. Mchoro Namba 3 hapa chini unatoa ufafanuzi zaidi.
Mchoro Namba 3:
Biashara Baina ya Zanzibar na Tanzania Bara: TZS.(Milioni )
         









Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020

       2.4   Hali ya Chakula na Bei katika Soko la Zanzibar :

32.    Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2019 Takwimu za uingizaji chakula kutoka nje zinaonesha kwamba jumla ya
Tani 100,331 za mchele, Tani 30,362 za sukari na Tani 41,904 za unga wa ngano zilikuwepo katika kipindi hicho kwa ajili ya matumizi ya soko la ndani, kama inavyoonekana katika Mchoro Namba 4 hapa chini.

Mchoro Namba 4:
Wastani wa Uingizaji wa Chakula Muhimukatika Soko la Zanzibar 2019 (Tani):
!

!
Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020

33.    Mheshimiwa Spika, Uwepo wa chakula pia ulichangiwa na uzalishaji wa bidhaa hizo nchini. Kwa kipindi cha Januari mpaka Oktoba 2019, uzalishaji wa Sukari nchini ulifikia tani 6,674 ambazo zilinunuliwa na kutumika ndani ya Zanzibar. Kwa upande wa unga wa ngano tani 37,143 zilizalishwa kwa kipindi cha Januari mpaka Disemba 2019.
34.    Spika, Bei za bidhaa muhimu kama za mchele na  unga wa ngano ziliongezeka kidogo katika soko la ndani kwa mwaka 2019 ukilinganisha na mwaka 2018.  Napenda kuliarifu Baraza lako tukufu kwamba Serikali inaendelea na utaratibu wa kusimamia bei za bidhaa muhimu (mchele, sukari na unga wa ngano) na kuangalia uwezekano wa kuongeza aina nyingine za bidhaa zinazowagusa sana wananchi. Kwa jumla wastani wa bei za reja reja za bidhaa muhimu kwa mwaka 2019 katika masoko ya Zanzibar ni kama zinavyoonekana katika Jadweli Namba 1 hapa chini:
Jadweli Namba 1:
Wastani wa Bei za Reja Reja za Chakula Muhimu katika Soko la Zanzibar:
(TZS/Kilo)
Bidhaa 
Julai - Sept
Okt – Dis
Jan – Machi
Mchele (Tulip,



Kasuku)
1,533
1,620
1,564
Basmati
3,726
3,714
3,714
Sukari
1,891 
1,893 
1,897 
Unga Ngano
1,363
1,387
1,387 
  Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020
3       HALI YA VIWANDA :
35.    Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa Viashiria vinavyotumika kupima maendeleo ya nchi duniani ni ukuaji na mchango wa Sekta ya Viwanda katika pato la Taifa. Wizara imeendelea kufanya juhudi mbali mbali kuhakikisha kwamba sekta ya viwanda inaimarika na mchango wake katika ujenzi wa uchumi unaongezeka siku hadi siku. Jitihada hizo ni pamoja na kutafuta wawekezaji kutoka nje ya nchi lakini pia kuwahamasisha wawekezaji wazalendo waweze kuanzisha viwanda. Lengo ni kuhakikisha bidhaa nyingi zaidi zinazalishwa hapa hapa nchini pamoja nakuongeza usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi kwa kutambua kwamba uchumi wa viwanda ndio uchumi imara zaidi (Stable Economy) na himilivu hata pale inapotokea  mdororo wa kiuchumi duniani (Economic Recession), kutokana na athari za majanga mbali mbali kama maradhi ya mripuko wa COVID-19 yaliyoikumba dunia hivi sasa.
36.    Mheshimiwa Spika, Mchango wa Viwanda katika pato la Taifa umeendelea kuongezeka kutoka asilimia 17.8 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 18.3 mwaka 2019 hii ni sawa na ongezeko la asilimia 0.5 iliyotokana na kufanya vizuri sekta ya uzalishaji Viwandani. Mripuko wa ugojwa wa COVID-19 umeonesha bayana umuhimu wa kuimarisha na kukuza viwanda vyetu ambapo jitihada zimeonekana.


Mchoro Namba 5:
Mchango wa Sekta za kiuchumi katika Pato la
37.    Mheshimiwa Spika, Sekta ya huduma ndiyo inayokuwa kwa kasi zaidi ukilinganisha na sekta nyengine za uchumi. Hali hii ni kutokana na kuimarika kwa sekta ya utalii na kuongezeka kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta hiyo. Hata hivyo kutokana na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kumesaidia sana kuongeza mchango wa sekta ya viwanda katika uchumi wetu. Juhudi hizo ni pamoja na kuanzisha kwa Wakala wa Kusimamia na Kuendeleza viwanda vidogo vidogo na vya kati (SMIDA), kupitisha Sera mpya ya Viwanda  pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji
kwa ujumla ambavyo vyote vimefanyika katika kipindi hiki cha awamu ya saba. 

38.    Mheshimiwa Spika, Hali ya uzalishaji bidhaa viwandani kwa mwaka 2019/2020 imeendelea kuimarika licha ya kuwepo kwa changamoto ya soko la Tanzania Bara kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu hapa Zanzibar. Tozo ya mifugo (livestock levy) ya shilingi 250 kwa lita moja ya maziwa yanayozalishwa na kiwanda cha ADPL kilichopo Fumba yanapoingia katika soko la Tanzania Bara imeathiri kwa kiwango kikubwa mauzo ya bidhaa hiyo na kusababisha kuporomoka kwa mapato ya kiwanda kiasi cha kushindwa kujiendesha kibiashara. Hivyo, athari ya tozo hiyo inapelekea maziwa ya ADPL kuwa ghali zaidi katika soko la Tanzania na kupoteza ushindani wa bei. Kwa mwaka 2019/2020 Kiwanda kimeweza kuzalisha lita 1,757,982 za maziwa ukilinganisha na lita 8,028,883 zilizozalishwa mwaka 2016/2017 na kulipa Shilingi milioni 315  kama mishahara ya wafanyakazi.

39.    Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Zanzibar Milling Corporation (ZMCL) kilichopo Mtoni kinachozalisha bidhaa ya unga wa ngano kimeendelea kuimarika kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya tani 27,070.1 za unga wa ngano na tani 6,690.72 za pumba (bran) zimeweza kuzalishwa na kuuzwa. 

40.    Mheshimiwa Spika, Uzalishaji katika kiwanda cha Sukari (ZSFL) kilichopo Mahonda umeendelea kuimarika kutokana na muitikio mzuri wa wananchi kulima miwa katika maeneo yao (Out growers) na kuiuza kiwandani hapo. Kutokana na matokeo hayo ya kupigiwa mfano kiwanda kimeweza kuvunja rekodi ya kuzalisha jumla ya tani 6,674 za sukari ambazo hazijawahi kuzalishwa kiwandani hapo tangu kiwanda hicho kilipoanza uzalishaji.  Vile vile kiwanda kimeweza kuzalisha lita 230,000 za spiriti (Rectified Ethanol) ambayo ni bidhaa muhimu katika kutengeneza viosha mikono (Sanitizer) na tani 3,600 za Molasses (Energy Concentrate) ambayo ni bidhaa muhimu kwa ajili ya kutengeneza virutubisho vya malisho ya mifugo hasa Ng’ombe.  Matarajio kwa mwaka 2020/2021 ni kuzalisha
tani 8,000 za sukari, lita 800,000 za spiriti na tani 4,500 za molasses.

41.    Mheshimiwa Spika, Kuongezeka kwa uzalishaji katika viwanda nchini kuna manufaa makubwa sana katika kukuza uchumi na maendeleo ya jamii (Socio-economic Development) ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbali na malipo ya mishahara kwa wafanyakazi viwandani; zaidi ya shilingi bilioni 3 zimekusanywa na Serikali kutokana na kodi na tozo mbali mbali kwa viwanda vitatu tu kama inavyoonekana katika kiambatanisho namba 1

42.    Mheshimiwa Spika, Mbali ya uwepo wa viwanda hivyo vikubwa, vipo viwanda vya kati ambavyo vimeanza uzalishaji katika kipindi cha 2019/2020. Miongoni mwa viwanda hivyo ni Turky Mifuko kinachozalisha mifuko (woven carrier bags) kilichopo Mgeni Haji chenye uwezo wa kuzalisha kilo 500,000 za mifuko kwa mwezi. Kiwanda kipya cha Zanto cha kusarifu tungule (Tomato Paste) na pili pili (Chilli Sauce) kilichopo Shakani, Kiwanda cha kuzalisha vifungashio (Messab Packaging) kilichopo Dimani, kiwanda cha kusarifu zao la chumvi kilichopo Kiembe Samaki, Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya nazi (Virgin Coconut Oil), Kiwanda cha kutengeneza mabati, Kiwanda cha kusarifu korosho na Kiwanda cha kuzalisha vifungashio vya kuhifadhia vyakula vilivyopo katika Eneo la Viwanda Amani (AIP).

43.    Mheshimiwa Spika, Baada ya Utangulizi na maelezo hayo ya awali kuhusu hali ya biashara na viwanda, naomba sasa niwasilishe utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na mwelekeo wa malengo ya mwaka 2020/2021.

4         UTEKELEZAJI WA BAJETI NA MIPANGO YA WIZARA KWA MWAKA 2019/2020:

4.1 Ukusanyaji wa Mapato:

44.    Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Biashara na Viwanda ilipangiwa lengo la kukusanya mapato ya shilingi bilioni 1.896 kutoka katika vyanzo vyake mbali mbali. Kwa kipindi cha miezi Tisa (Julai 2019 – Machi 2020), Wizara ilikadiria kukusanya mapato ya shilingi bilioni 1.467. Hadi kufikia mwezi wa Machi, 2020, jumla ya shilingi milioni 600.13 zilikwishapatikana ikiwa ni sawa na asilimia 41 ya makisio ya makusanyo ya miezi tisa na kuingizwa katika Mfuko mkuu wa Serikali. 

45.    Mheshimiwa Spika, Kati ya fedha hizo jumla ya shilingi milioni 41.3 zilipangwa kukusanywa kwa upande wa Ofisi kuu Pemba, hadi kufikia 31 Machi, 2020 jumla ya shilingi milioni 28.09 zimekusanywa ikiwa ni sawa na asilimia 68 ya fedha zilizopangwa kwa kipindi hiki. Kwa upande wa Idara ya Biashara na Ukuzaji Masoko kupitia kitengo cha Vipimo na Mezani kilipanga kukusanya Shilingi milioni 525.57 hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2020 jumla ya shilingi milioni
56.01 zimekusanywa sawa na asilimia 11 ya makadirio ya mapato hayo.
 Aidha, Taasisi ya Viwango (ZBS) ilipangiwa kukusanya Shilingi milioni 545.00 kutoka katika malipo ya usimamizi wa viwango, hadi kufikia 31 Machi, 2020 jumla ya Shilingi milioni 295.86 zimekusanywa sawa na asilimia 54 ya mapato kwa kipindi hiki. Kadhalika, Wakala wa Usajili Biashara na Mali (BPRA) ilipanga kukusanya Shilingi milioni 355.30 kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato kwa huduma inazotoa, hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2020 jumla ya Shilingi milioni 220.17 sawa na asilimia 62 zimekusanywa kwa kipindi hiki.

46.    Mheshimiwa Spika, Mchanganuo wa Mapato hayo kwa kipindi cha Julai 2019 - Machi 2020, ni kama unavyoonekana katika Jadweli Namba 2 hapa chini;


47.  Mheshimiwa Spika, Sababu kubwa ya kushuka kwa mapato kwa kipindi cha mwaka 2019/2020, ni kutokana na kupungua kwa kazi usajili na gharama za malipo ya maombi mapya ya biashara na kufanya mapitio ya taratibu za usajili na gharama zake. Aidha, kwa kipindi cha robo ya tatu (Januari – Machi), biashara kwa ujumla imeathirika kutokana na mripuko wa ugonjwa wa COVID – 19 ambao umesababisha kupungua kwa makampuni ya nje ya nchi yanayoshajihisha biashara ya huduma na bidhaa nchini.

4.2  Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/ 2020:

48.    Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Biashara na Viwanda, iliidhinishiwa matumizi ya jumla ya Shilingi bilioni 15.597 kwa ajili ya kutekeleza program kuu nne (4) na  program ndogo kumi (10). Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 7.547 zilipangwa kutumika kwa ajili ya kazi za kawaida na shilingi bilioni 8.050 kwa kazi za maendeleo. Hadi kufikia Machi 2020, Wizara iliingiziwa jumla ya Shilingi bilioni 6.25 ambazo ni sawa na asilimia 40 ya bajeti ya mwaka. Mchanganuo wa matumizi hayo kwa kila program ulikuwa kama unavyoonekana katika Kiambatanisho Namba 2.

49.    Mheshimiwa Spika, Sababu kubwa ya matumizi ya asilimia 40 ni kuchelewa kwa upatikanaji wa fedha za kuwaendeleza wajasiriamali (Khalifa Fund), upatikanaji wa fedha za kuendeleza maeneo ya viwanda pamoja na utekelezaji wa miradi mingine ya Wizara inayohusu ujenzi kuchukua muda mrefu kutokana na taratibu zake. Miradi yenyewe ni ujenzi wa Maabara na Afisi za Taasisi ya Viwango (ZBS) na ujenzi wa Afisi za Wakala wa Kusimamia na Kuendeleza Viwanda vidogo vidogo na vya kati (SMIDA). 

         Mheshimiwa Spika,  Matarajio ni kuwa kabla ya kumalizika mwaka wa fedha 2019/2020 utekelezaji utaongezeka kwa asilimia kubwa zaidi.

4.3    Utekelezaji wa Malengo ya Wizara :

50.    Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Biashara na Viwanda ulifanyika kulingana na huduma na shughuli zilizowekwa katika programu za Wizara kama ifuatavyo:

PROGRAMU KUU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA:

51.    Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda imeundwa na Programu ndogo tatu ambazo ni Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara; Programu ndogo ya Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti; na Programu ndogo ya Uratibu na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara Pemba. Katika kutekeleza majukumu yake, program hii ilipangiwa matumizi ya Shilingi bilioni 2.99 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Napenda kuliarifu Baraza lako tukufu kwamba, hadi kufikia Machi 2020, programu hii imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni 2.31 ikiwemo mishahara na kazi nyengine za uendeshaji sawa na asilimia77 ya makadirio ya mwaka. Utekelezaji wa huduma zilizopangwa katika kila program ndogo nilizozitaja ni kama ifuatavyo:

Programu ndogo ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara:

52.    Mheshimiwa Spika, Programu hii ndogo ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara inasimamiwa na Idara ya Uendeshaji na Utumishi. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, programu hii ndogo ilikuwa na jukumu la kutoa huduma ya ununuzi wa vifaa vya ofisi na usafiri pamoja na huduma ya usimamizi wa rasilimali watu na huduma kwa ujumla ambayo inahusisha kazi za uimarishaji wa mazingira mazuri ya kufanyia kazi, utoaji wa huduma kwa Idara zote za Wizara na uratibu wa mikutano ya majadiliano ya ndani, ya Kikanda na ya Kimataifa. Program hii ndogo ilipangiwa matumizi ya shilingi bilioni 2.14 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni 1.74 ikiwemo mishahara na kazi nyengine za uendeshaji sawa na asilimia 81 ya makadirio ya mwaka. Huduma za Program ndogo ya
Utawala na Uendeshaji zilitekelezwa kama ifuatavyo:-
Usimamizi wa Rasilimali Watu na Huduma kwa Ujumla:

53.    Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha mazingira ya utendaji kazini, Wizara imeendelea kuwalipa mishahara wafanyakazi 217 (Wanaume 108, Wanawake 109) pamoja na stahiki zao kwa mujibu wa muundo wa malipo wa Serikali. Aidha, Wizara imefanya maombi Tume ya Utumishi Serikalini ya kubadilishwa kada wafanyakazi watano (5) baada ya kurudi masomoni na mfanyakazi mmoja (1) tayari ameshabadilishwa. Kadhalika, Wizara iliwapatia likizo na stahiki zao wafanyakazi 38, kati ya hao wafanyakazi 25 wamepatiwa likizo la kawaida, 9 likizo la dharura na 4 likizo la uzazi pamoja na kumpatia mfanyakazi mmoja (1) gharama za mazishi. Pamoja na hayo, Wizara imeajiri wafanyakazi wapya 44 katika fani ya Uchumi, Biashara, Utawala, Ununuzi, Sheria, Uhandisi na Katibu muhtasi.

54.    Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake kulingana na mahitaji husika ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mfanyakazi mmoja (1) amepatiwa mafunzo ya muda mrefu katika fani ya Uchumi. Wafanyakazi nane (8) wanaendelea na masomo katika fani ya Uchumi, Takwimu na uendeshaji, Secretarial management, Maendeleo ya miji (Rural/Urban Development) na Utawala katika ngazi ya Uzamili na Uzamivu.

 Aidha, Wizara imewapatia mafunzo ya muda mfupi na elekezi wafanyakazi 40, kati ya hao wafanyakazi thelathini na nne (34 waajiriwa wapya) mafunzo elekezi, watano (5) mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu na Mfanyakazi mmoja (1) mafunzo ya Udereva.

55.    Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea Kuratibu na kushiriki mikutano ya majadiliano ya biashara na viwanda ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Wizara ilishiriki Mikutano tisa
(9) ya majadiliano ya biashara katika ngazi za wataalamu
na Mawaziri. Mikutano hiyo ni Mkutano wa mafunzo ya sheria na uchunguzi wa alama za biashara nchini Korea, Mkutano wa ushiriki wa kuendeleza viwanda vya nguo kanda ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Mkutano wa soko la pamoja la Afrika (Africa Continental Free Trade Agreement (AFCFTA) nchini Ethiopia na Mkutano wa kufanya tathmini ya gharama za uzalishaji wa bidhaa ya sukari nchini Msumbiji, Ethiopia, Dar-es- Salaam na Dodoma.
Huduma ya Ununuzi wa Vifaa vya Ofisi
56.    Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha mazingira mazuri ya ufanyaji kazi na upatikanaji wa huduma kwa wakati kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara imeendelea kufanya ununuzi kwa kuzingatia mpango wa manunuzi wa mwaka. Manunuzi hayo ni pamoja na vifaa vya kuandikia, mafuta, vifaa vya usafiri, Komputa na vifaa vyake pamoja na vifaa vya usafiri. Aidha, Wizara imefanya ukarabati wa jengo la Ofisi kuu kwa kupaka rangi, marekebisho ya mfumo wa maji safi na maji taka na eneo la maegesho ya magari, matengenezo ya umeme na ukarabati mdogo mdogo.
 Programu ndogo ya Uratibu wa Mipango, Sera na
Tafiti za Wizara:

57.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti ilikuwa na jukumu la kutayarisha, kuchambua na kutathmini utekelezaji wa mipango na malengo  maalum ya Wizara. Huduma  ambazo zimesimamiwa  na  Programu hii ndogo  ni Uandaaji na Uibuaji wa Sera na Tafiti za Wizara, Uandaaji na Utekelezaji wa Mipango ya Wizara na Usimamizi wa Takwimu  za Biashara na Viwanda. Program hii ndogo ilipangiwa matumizi ya shilingi  milioni 367.12 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 235.55 milioni ikiwemo mishahara na kazi nyengine za uendeshaji sawa na asilimia 64 ya makadirio ya mwaka. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa programu  hii ndogo, huduma ambazo nimezitaja hapo juu zimetekelezwa kama ifuatavyo: -
Uandaaji na Uibuaji wa Sera na Tafiti za Wizara
58.    Mheshimiwa Spika, Katika kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na uwekezaji, Wizara imeandaa na kuwasilisha Serikalini Sera ya Maendeleo ya Sekta Binafsi kwa madhumuni ya kuikuza na kuisimamia sekta binafsi ili iweze kuongeza tija na kushiriki katika maendeleo ya nchi. Sera hii imepitishwa na kukubalika ianze utekelezaji wake mara moja. Aidha, Wizara imefanya uzinduzi wa Sera ya Viwanda ya mwaka 2019/2029. Kwa hatua nyingine, Wizara imefanya mapitio ya Sera ya Biashara ya mwaka 2006 na ipo katika hatua za mwisho za kuiwasilisha Serikalini.

59.    Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha utafiti mdogo wa  Mahitaji ya soko la Uyoga (Demand for Mushroom). Matokeo ya utafiti huo yameonesha kwamba mahitaji ya uyoga kwa mwezi ni kilo 3,840 ambapo uzalishaji wa ndani
ni kilo 12. Aidha, utafiti umeonesha kwamba asilimia 64 ya Hoteli zinatumia uyoga wa Viwandani (Canned) kutoka nje ya nchi na asilimia 26.15 zinatumia uyoga asili na asilimia 9.23 hazitumii uyoga katika menu zao. Uyoga wa asili unaotumika kwa wingi Zanzibar ni aina ya ‘Oyster’, ‘Button’ na Portobello”. Utafiti umeonesha kuwepo na soko kubwa la zao la uyoga hasa katika sekta ya utalii. Aidha, Wizara itawasilisha matokeo hayo Tume ya Mipango na kwa wadau ili kuhamasisha uzalishaji wake hapa Zanzibar.
Uandaaji na Utekelezaji wa Mipango ya Wizara
60.    Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Wizara tuliopanga kwa mwaka wa fedha 2019/2020 yamefikiwa, Wizara imeandaa mpango kazi wa Wizara na mpango wa ufuatiliaji na tathmini kwa kazi za maendeleo. Aidha, ripoti za utekelezaji wa miradi na kazi za kawaida kwa kila kipindi cha robo mwaka zimeandaliwa pamoja na kuandaa vipaumbele kwa sekta ya Biashara na Viwanda kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Usimamizi wa Takwimu za Biashara

61.    Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya utafiti mdogo (survey) ya kupima soko la bidhaa za viwanda (Maji), pamoja na mambo mengine, soko kuu la bidhaa ya maji inayozalishwa ni hapa hapa Zanzibar. Utafiti umeonesha gharama kubwa za usafirishaji; alama ya ubora ya Taasisi ya Viwango ya Tanzania Bara na cheti cha Wakala wa Chakula
na Madawa ya Tanzania bara pamoja na vibali mbali mbali ni miongoni mwa vikwazo vinavyoikumba bidhaa ya maji kupata soko nje ya Zanzibar.

62.    Mheshimiwa Spika, Katika usimamizi wa Takwimu, Wizara imekusanya na kuzihifadhi Takwimu za bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania bara zikiwemo bidhaa za vyakula, mboga, vyombo vya usafiri na vinywaji. Takwimu hizo hukusanywa kila mwezi kupitia Bandari zetu za Malindi, Wesha, Wete na Mkoani. Aidha Takwimu zilizokusanywa zimewasilishwa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa uchambuzi zaidi.

Programu ndogo ya Uratibu na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara Pemba:

63.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ofisi Kuu Pemba ina jukumu la kutekeleza na kusimamia shughuli zote za Wizara ya Biashara na Viwanda kwa upande wa Pemba. Programu hii ndogo ilipangiwa matumizi ya shilingi milioni 485.99  kwa mwaka wa fedha 2019/2020, na hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 342.36 ikiwa ni mishahara na kazi nyengine za kawaida sawa na asilimia 70 ya makadirio ya mwaka. Huduma iliyopangwa kutolewa na Programu hii imetekelezwa kama ifuatavyo:-

Uratibu wa Shughuli za Wizara Pemba

64.    Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza huduma hii,
Wizara ilifanya shughuli mbali mbali zikiwemo;
i.         Utoaji wa huduma na ununuzi wa vifaa ambapo Wizara kupitia Afisi Kuu Pemba ilifanya ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi, ununuzi wa huduma za umeme, maji na mawasiliano, ununuzi wa gari moja (1), ununuzi wa mafuta na kutoa huduma ya usafiri kwa maafisa wa Wizara kwa ajili ya ufuatiliaji wa kazi mbali mbali za Wizara;
ii.        Usimamizi rasilimali watu na huduma kwa ujumla katika kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa stahiki zao, Wizara kupitia Ofisi kuu Pemba imewapatia likizo jumla ya Wafanyakazi 23. Aidha, Afisi imewapatia mafunzo elekezi waajiriwa wapya 7 kwa lengo la kuwaongezea ufanisi katika kazi;
iii.      Katika hatua ya kuwakuza na kuwaendeleza wajasiriamali Wizara kupitia Afisi Kuu Pemba ilitembelea jumla ya vikundi 84 vya wajasiriamali na kuandaa mikutano mitatu (3) lengo ni kusikiliza changamoto zao na kuweza kuzitatua katika Wilaya zote za Pemba. Kati ya vikundi hivyo, arobaini na nane (48) vilipatiwa mafunzo ya utengenezaji sabuni, vikundi kumi (10) vilipelekwa Tanga kujifunza kivitendo kuhusu usarifu wa bidhaa za viungo na vikundi kumi
na sita (16) vilishiriki katika maonesho ya saba saba Tanzania Bara na Tamasha la Biashara la Zanzibar.
iv.      Kufanya ukaguzi wa mizani na vipimo kwa mujibu wa Sheria ambapo jumla ya mizani 662,  mita ndogo za mafuta 44, mita 3 kubwa za kutolea mafuta katika bandari ya Wesha, magari 8 ya kubebea mafuta na matangi 4 ya mafuta ya chini yamekaguliwa katika shehia mbali mbali za Wilaya zote za Pemba na;
v.        Kufanya ukaguzi wa maduka, maghala na bekari. Katika ukaguzi huo jumla ya maduka 1,906 maghala 31 na bekari 42 zimekaguliwa. Kaguzi zote hizi hufanyika ikiwa ni sehemu za hatua za kuwalinda watumiaji kwa kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa zinazouzwa.

PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA VIWANDA NA UJASIRIAMALI:

65.    Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali ambayo utekelezaji wake unasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Viwanda na Wakala wa Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo, vidogo na vya kati (SMIDA) inajumuisha Programu ndogo mbili ambazo ni Ukuzaji Viwanda na Maendeleo ya Ujasiriamali. Program hii kuu ilipangiwa jumla ya shilingi bilioni 6.85kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii kuu imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni
1.08 ikiwemo mishahara, kazi za maendeleo na kazi nyengine za kawaida, sawa na asilimia 16 ya makadirio ya mwaka. Sababu ya asilimia ndogo ya utekelezaji ni kama nilivyoeleza awali wakati natoa ufafanuzi wa matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Program ndogo hizo utekelezaji wake ni kama ifuatavyo:-
Programu Ndogo ya Ukuzaji Viwanda

66.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ukuzaji Viwanda ina jukumu la kutoa huduma ya kuimarisha sekta ya viwanda. Program hii ndogo ilipangiwa jumla ya shilingi bilioni 3.29 kwa mwaka wa fedha 2019/2020, na hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni 1.06 ikiwemo mishahara, kazi za maendeleo na kazi nyengine za kawaida, sawa na asilimia 32 ya makadirio ya mwaka. Utekelezaji wa program ndogo ya Ukuzaji Viwanda ulikuwa kama ifuatavyo:-

Uimarishaji wa Sekta ya Viwanda

67.    Mheshimiwa Spika, Katika kurahisisha na kuweka mazingira mazuri ya uekezaji katika sekta ya viwanda, Wizara kwa kushirikiana kampuni ya Kunshan Asia Aroma wamefanya ukarabati mkubwa wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya makonyo huko Wawi, sambamba na kukamilisha ujenzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha mafuta ya mimea yakiwemo mkaratusi, mchaichai, mrehani na mdalasini. Kutokana na ukarabati huo, Viwanda hivyo vina uwezo wa kuzalisha tani 300 za mafuta ya makonyo na tani 300 za mafuta ya mimea kwa mwaka. Kazi inayoendelea hivi sasa ni kuimarisha mashamba kwa ajili ya kupata malighafi za kulisha viwanda hivyo.

68.    Mheshimiwa Spika, Kadhalika, katika hatua za kuliendeleza zao la mwani Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kushirikiana na wawekezaji kutoka Indonesia imeandaa andiko la mradi (feasibiliyy study) kwa ajili ya uanzishaji wa kiwanda cha kusarifu zao la mwani kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Viwanda Chamanangwe Mkoa wa Kaskazini Pemba. Hatua inayofuata hivi sasa ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi na taratibu za ununuzi wa mashine za kiwanda.

69.    Mheshimiwa Spika, Hatimaye, “hayawi hayawi sasa yamekuwa” kwa upande wa Kiwanda kipya cha nguo, kwa sasa kipo katika hatua za mwisho kabisa katika kukamilisha ujenzi na ufungaji mitambo. Huu ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya viwanda hapa nchini na Kampuni ya Basra Textiles Mills Co. Limited iliyosajiliwa hapa Zanzibar. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita 200,000 kwa siku za vitambaa aina ya Khanga, vitenge, mashuka pamoja na vitambaa vya aina mbali mbali kulingana na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Ni matarajio yetu kwamba, jumla ya wafanyakazi 500 wa kudumu watapata ajira katika kiwanda hicho vile vile uwepo wake pia utapelekea eneo la Chumbuni kuwa ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kiuchumi hapa nchini.

70.    Mheshimiwa Spika,  Aidha, Wizara   inaendelea kurahisisha uwekezaji wa Viwanda na kupunguza changamoto zilizopo  kwa  kuiombea hati ya  ukodishaji ardhi (land lease) Kampuni ya AKM Glitters limited inayojihusisha na uzalishaji  wa chakula cha kuku na chinjio la kisasa katika eneo la shamba la Hanyegwa mchana. Lengo ni kuanza ujenzi wa shamba la kuku mama (incubator) la kutotolea vifaranga, kiwanda cha chakula cha kuku pamoja na chinjio la kisasa (An Integrated Project) ili kuzalisha bidhaa ambayo itakuwa na viwango vya kimataifa kwa ajili ya soko la ndani, utalii na nje ya nchi. Aidha, Kampuni hiyo tayari imekamilisha hatua zote za usajili  kama mwekezaji wa mradi na kazi inatarajiwa kuanza wakati  wowote atakapopatiwa hati hiyo.

71.    Mheshimiwa Spika, Katika kuyaendeleza maeneo maalum ya Viwanda (Industrial Parks) kwa kila Mkoa, kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Biashara na Viwanda imekamilisha sehemu kubwa ya ulipaji wa fidia wa eneo la Viwanda la Chamanangwe, jumla ya Wananchi 127 wenye mashamba madogo na makubwa katika shehia ya Kiuyu na mchanga mdogo wamelipwa. Pamoja na kuandaa Mpango wa matumizi (Master Plan) wa eneo la Chamanangwe. Pia, Wizara imefanya uchambuzi wa utendaji wa Viwanda (Industrial Perfomance) kwa Viwanda saba vya kimkakati vilivyochaguliwa ambavyo ni Kiwanda cha Sabuni (Inaya Company LTD), Kiwanda cha Sukari Mahonda (Zanzibar Sugar Factory), Kiwanda cha Maziwa (Azam Diary Milk), Kiwanda cha Mifuko (Turky Mifuko), Kiwanda cha Tishu (Allawi Supply LTD), Kiwanda cha Chumvi (Swahili Coast Salt Company) na Kiwanda cha Unga (Zanzibar Milling Company LTD) ili kuviendeleza na kuvilinda kwa kuainisha changamoto zinazovikabili Viwanda hivyo. Hata hivyo, kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara inaendelea na kazi hii kwa kuangalia kwa kina changamoto zilizopo.
72.    Mheshimiwa Spika, Wizara imeratibu na kushiriki katika Maonesho ya 4 ya Bidhaa za Viwanda kwa kushirikiana na Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) yaliofanyika kuanzia tarehe 5-9 Disemba, 2019 katika Viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam. Aidha, Viwanda vitatu (3) vilishiriki katika maonesho hayo ikiwemo Kiwanda cha Sukari Mahonda, Kiwanda cha Sabuni (ZANOP) na Kiwanda cha Nguo (Zanzibar Apparel Co Ltd).
73.    Mheshimiwa Spika, Katika kuongeza thamani kwa bidhaa zinazozalishwa Zanzibar, Wizara imetenga na kuandaa eneo la ujenzi (Site Plan) kwa ajili ya kusarifu zao la chumvi katika eneo la Chamanangwe-Pemba. Kwa sasa Kampuni ya Zanzibar Coast Salt Company Limited tayari imeshaanza kuzalisha kwa majaribio bidhaa ya chumvi za aina nane kwa matumizi mbali mbali na kuuza katika masoko ya kitalii.  Bidhaa hizo zimetengenezwa kwa kuwekwa viungo mbali mbali na kupewa majina ya Choma, Kichaa, Zabibu, Kali, Nyota, Cheza, Tikisa na Kila siku. Kwa sasa timu ya wataalamu kutoka Uingereza inaendelea na kuandaa mpango mkakati wa kuongeza uzalishaji chumvi ili kukidhi mahitaji ya kiwanda.

74.    Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhamasisha na kusimamia uanzishwaji wa viwanda vingine mbalimbali katika sekta za chakula, vifaa vya ujenzi na ushoni. Kiambatanisho Nambari 3 Kinaonesha baadhi ya Viwanda na hatua mbali mbali za uanzishaji wake kwa kipindi cha mwaka 2019/2020.

75.    Mheshimiwa Spika, Kama tunavyoelewa Wakala wa Kusimamia na Kuendeleza Viwanda Vidogo vidogo, vidogo na vya Kati (SMIDA) bado ni taasisi mpya na inahitaji Ofisi na eneo la kufanyia kazi. Kwa sasa imefanya ukarabati wa majengo yalikuwepo hapo Maruhubi. Kwa mwaka 2019/2020, Wizara ilipanga kujenga Ofisi ya makao makuu ya Wakala katika eneo la Maruhubi. Napenda kulijulisha Baraza lako kuwa hatua za Zabuni za kumpata Mshauri elekezi na Mkandarasi zimekamilika. Kwa sasa Serikali inaandaa mkataba ili kazi za ujenzi ianze mara moja.

76.    Mheshimiwa Spika, Wakala kwa kushirikiana na Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Trust ya Tanzania imeingia makubaliano (MoU) ya kuanzisha kituo cha usarifu wa mazao ya kilimo Zanzibar “Agribusiness Innovation Centre”. Matengenezo ya kituo hicho tayari yameshaanza katika eneo la Maruhubi. Wakala inatarajia kuanzisha viwanda vidogo vidogo 25 vya mfano na kukabidhiwa vijana waviendeshe chini ya usimamizi wa PASS na SMIDA. Aidha, mafunzo ya utengenezaji wa vitambaa vya vikoi, usarifu wa matunda, utengenezaji wa dawa ya kutakasa mikono (sanitizer) yametolewa na uzalishaji umeanza kwa wajasiriamali lengo ni kuzalisha bidhaa zenye ubora na zitakazoweza kuuzika katika masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na mafunzo ya udhibiti wa fedha za miradi kwa wajasiriamali kwa Unguja na Pemba.

77.    Mheshimiwa Spika, Katika kukuza na kuendeleza vipaji vya ubunifu kwa wajasiriamali, Wakala imeandaa na kufanya mashindano ya ubunifu kwenye Tamasha la Sita (6) la Biashara lililofanyika kuanzia tarehe 2-15 Januari, 2020. Jumla ya wabunifu 44 walitembelewa, kati ya hao wabunifu 30 waliteuliwa kushiriki katika mashindano hayo. Wabunifu tisa (9) walipata zawadi pamoja na ushauri wa jinsi ya kukuza bunifu zao kwa ajili ya kuleta tija kwa maendeleo ya Viwanda Zanzibar. Sambamba na kuvitembelea viwanda 185, kuvipatia ushauri wa kitalaamu na kutengeneza mashine tano (5) za teknolojia rahisi waliopatiwa wazalishaji.

78.    Mheshimiwa Spika, Wajasiriamali tisa (9) wamepatiwa mikopo yenye jumla ya TZS shillingi 100,000,000. Mikopo iliyotolewa ni kwa ajili ya kununulia mashine ya kutengenezea chakula cha kuku; Mashine ya kufumia vikoi; Ununuzi wa vifungashio; Ununuzi wa vifaa vya bekari na Jenereta; Mashine ya kutotolea vifaranga; na Uimarishaji wa kilimo cha mbogamboga. Jumla ya Shilingi milioni 35.66 tayari zimerejeshwa. Aidha, Wakala wamefanya makongamano mawili (2) yenye lengo la kujadili changamoto za viwanda na taasisi zinazohusiana moja kwa moja na wajasiriamali. Matokeo ya makongamano hayo ni pamoja na kuandaa programu ya pamoja itakayowezesha kuwapatia huduma wajasirimali wenye viwanda vidogo vidogo na vya kati katika sehemu moja “One Stop Center” pamoja na “Business
Clinic”.
79.    Mheshimiwa Spika, Katika kutatua changamoto ya vifungashio kwa Wajasiriamali Wakala wameagiza vifungashio 10,000 vya maziwa pamoja na machine 5 za vifungashio, ili kuwasaidia wajasirimali wenye viwanda wa sekta ya maziwa kuweza kubadilisha vifungashio kama walivyoelekezwa na Wakala wa dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA). Kadhalika, Wakala imekamilisha Muundo wa utumishi na muundo wa mishahara ambao unaendana na Muundo mpya wa Wakala ulioidhinishwa na Serikali.
          Programu ndogo ya Maendeleo ya Ujasiriamali
80.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Maendeleo ya Ujasiriamali ilipangiwa jumla ya shilingi bilioni 3.57kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 21.11 kwa kazi za kawaida, sawa na asilimia 1 ya makadirio ya mwaka. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali kuwa fedha za miradi zilizotarajiwa katika program hii ndogo ni kutoka washirika wa maendeleo (Khalifa fund) ambazo hazikupatikana kwa mwaka huu wa fedha. Utekelezaji wa program ndogo ya Maendeleo ya
Ujasiriamali ulikuwa kama ifuatavyo:-

Kutoa msaada kwa Wajasiriamali

81.    Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha rasimu ya mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Ujasiriamali (MSME’s) ambapo mapitio yake  yamezingatia mambo mapya yanayokwenda sambamba na wakati na mabadiliko ya kiujasiriamali yanayotokea duniani, pamoja na kutoa muongozo wa kuendeleza na kusimamia sekta ya ujasiriamali nchini kupitia mikakati mipya iliyowekwa.

82.    Mheshimiwa Spika, Katika kusimamia utekelezaji wa sera ya SME’s Wizara imefanya vikao viwili vya Kamati ya ushauri ya Ujasiriamali ambayo inaundwa na wajumbe kutoka sekta ya umma na sekta binafsi. Kupitia vikao hivyo wajumbe walijadiliana juu ya kazi za wajasiriamali na mafanikio yao, changamoto wanazokumbana nazo pamoja na kutoa ushauri serikalini juu ya namna bora ya kuendeleza sekta ya ujasiriamali.  Pamoja na hayo, imeonekana kwamba kuna mwamko mkubwa wa wananchi hasa vijana kujiajiri katika shughuli za ujasiriamali hasa kilimo na uzalishaji bidhaa. Miradi ya wajasiriamali imeanzishwa kwa ushirika au vikundi vya uzalishaji.

83.    Mheshimiwa Spika, Jumla ya miradi 100 ya vikundi vya Wajasiriamali na wenyeviwanda vilikaguliwa ikiwemo miradi ya uzalishaji viungo, chumvi, sabuni, uhunzi, utengenezaji matofali na kokoto, miradi ya viwanda vya useremala, wazalishaji dagaa, maji na vyakula kwa ajili ya kupatiwa ushauri wa kitaalamu na kukusanya taarifa zao. Lengo ni kufanya ufuatiliaji na kutathmini hali ya sasa ya sekta ya viwanda kwa mwaka 2019/2020 ukilinganisha na mwaka uliopita 2018/2019 pamoja na kuainisha changamoto zao. Ukaguzi ulionesha, Viwanda 70 kati ya hivyo vipo katika uzalishaji wa bidhaa (manufacturing/processing) na 30 vipo katika uchimbaji (mining and quarying). Asilimia 95 ya viwanda hivyo vinamilikiwa na wazawa vimeajiri wafanyakazi wapatao 1,359 na asilimi 5 iliyobaki ya Viwanda vinamilikiwa na wageni vimeajiri wafanyakazi 90.

84.    Mheshimiwa Spika, Sekta ndogo ya uchimbaji katika viwanda vinavyotegemea malighali ya mchanga, jasi  na kokoto kwa mwaka 2019/2020 imeshuka kutoka TZS Bilioni 6.23 mwaka 2018/2019 hadi TZS Billioni 4.48 mwaka 2019/2020 sawa na upungufu wa asilimia 28. Aidha, idadi ya ajira imeshuka kutoka wafanyakazi 325 mwaka 2018/2019 hadi wafanyakazi 256 mwaka 2019/2020 sawa na anguko la asilimia 21, hali hiyo imetokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ndogo ya uchimbaji (mining and quarying).
      
               PROGRAMU KUU YA UKUZAJI NA UENDELEZAJI WA BIASHARA:

85.    Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Ukuzaji na Uendelezaji wa Biashara inajumuisha Programu ndogo nne (4) ambazo ni Ukuzaji wa Masoko na Usafirishaji, Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji, Urahisishaji wa Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani pamoja na Usajili
wa Biashara na Mali. Programu hii ilipangiwa matumizi ya shilingi bilioni 3.03 kwa mwaka wa fedha 2019 /2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni 1.79 ikiwemo mishahara, ruzuku, miradi na kazi nyengine za uendeshaji, sawa na asilimia 59 ya makadirio ya mwaka. Utekelezaji wa kazi zilizopangwa katika kila program ndogo nilizozitaja ni kama ifuatavyo:
 Programu ndogo ya Ukuzaji wa Masoko na
Usafirishaji
86.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ukuzaji wa
Masoko na Usafirishaji inasimamiwa na Idara ya Biashara na Masoko. Huduma ambazo zimesimamiwa na kutekelezwa na Programu hii ndogo ni uimarishaji wa mazingira mazuri ya biashara pamoja na kuongeza Fursa za Masoko na Urahisishaji Biashara.
 Program hii ndogo ilipangiwa jumla ya shilingi milioni 754.86 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 393.45 kwa ajili ya mishahara, kazi za maendeleo na kazi nyengine za kawaida sawa na asilimia 52 ya makadirio ya mwaka. Utekelezaji wa huduma za program ndogo hii ni kama ifuatavyo;
Fursa za Masoko na Urahisishaji Biashara
87.    Mheshimiwa Spika, Mojawapo ya jukumu muhimu la
Wizara ya Biashara na Viwanda ni kuzitafutia masoko bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuangalia changamoto zilizopo katika masoko hayo. Katika hatua tunazozichukua ni kuandaa, kuratibu na kushiriki katika maonesho na matamasha mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara iliratibu ushiriki wa Zanzibar katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba) yaliyofanyika Dar es Salaam mwezi wa Julai 2019. Taasisi saba (7) za Serikali zilishiriki katika maonesho hayo ambazo ni Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC), Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), Kamisheni ya Utalii (ZCT), Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi ya Zanzibar (ZIPA), Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni, Wakala wa Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo na vya Kati (SMIDA) pamoja na wajasiriamali 37 kutoka Unguja na Pemba. Bidhaa ambazo zilioneshwa na wajasiriamali walioshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na bidhaa za kusindika, vyakula vikavu, kazi za mikono, sabuni, dawa za asili, bidhaa za viungo (spices), mafuta ya mimea na nyenginezo. Aidha, Maonesho ya Sabasaba yaliweza kutoa fursa kwa wajasiriamali wetu kutangaza bidhaa zao na kuweza kupata wateja wengi zaidi.
88.    Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanapata masoko ya uhakika ya bidhaa zao, Wizara pia iliratibu na kutayarisha Tamasha la Biashara ambalo hufanyika kila mwaka ifikapo Januari ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa mwaka huu Tamasha hili lilikuwa ni la sita ambalo lilijumuisha jumla ya washiriki 389 kati ya hao, kutoka Tanzania bara 51, Kenya 3, Burundi 4, Rwanda 6, Uganda 1, Misri 2 na Uturuki 1. Mauzo yaliyofanyika katika Tamasha hilo ni wastani wa Shilingi milioni 954.68

Aidha, Tamasha hilo la sita (6) la biashara, Wizara pia iliandaa majadiliano katika siku maalum 3 zilizowekwa kwa madhumuni ya kutoa nafasi kwa wafanyabiashara na Taasisi kuweza kujadiliana kuhusiana na ukuzaji wa sekta ya biashara. Siku hizo ni siku ya Ubunifu (Innovation Day), Siku ya bidhaa za kimkakati  na Kliniki ya Biashara ambapo ilizinduliwa rasmi siku hiyo. Lengo kuu la kuweka siku hizi ni kuweza kuwakutanisha watumiaji, wazalishaji wa bidhaa pamoja na Taasisi zinaohusika na maswala ya biashara na uzalishaji kufanya majadiliano, kuibua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wazalishaji, na kutoa mapendekezo katika kuboresha sekta ya biashara na uzalishaji nchini. Aidha majadiliano hayo yameweza kutoa miongozo na maelekezo mbali mbali ambayo yatawasaidia wazalishaji kwa ujumla.

89.    Mheshimiwa Spika, Vile vile, Wizara imeratibu na kushiriki katika maonesho ya biashara ya kusherekea kutimia miaka 20 ya maonesho ya Kikanda ya Jua kali/Nguvu Kazi yaliyofanyika Fumba Zanzibar kuanzia mwezi Novemba, 2019. Madhumuni ya maonesho haya ni kuhakikisha kuwa Wajasiriamali wanapata fursa za kuzitangaza bidhaa zao katika masoko ya Afrika Mashariki. Zaidi ya Wajasiriamali 120 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar walishiriki katika maonesho haya ambayo hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya nchi katika Jumuiya.

90.    Mheshimiwa Spika, Wizara katika hatua ya kuimarisha Mashirikiano ya kibishara ya Kikanda na Kimataifa imeweza kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kikanda na kimataifa yanayohusiana na maswala ya Biashara ambapo Mikutano hiyo ni pamoja na vikao vya majadiliano ya uanzishwaji wa biashara huru barani Afrika (Continental Free Trade Africa), vikao vya itifaki ya biashara ya huduma Afrika Mashariki, vikao vya kuondosha vikwazo visivyo vya kiushuru (NTBs), vikao vya urahisishaji biashara (Trade Facilitation), vikao vya usimamiaji wa maswala ya TBT na SPS  kwa lengo la kurahisisha ufanyaji biashara katika soko la kikanda na Kimataifa. Katika mikutano fursa na changamoto mbali za kibiashara za kikanda na kimataifa ziliweza kujadiliwa na baadhi yake kupatiwa maamuzi katika ngazi za Wakuu wa Nchi.

91.    Mheshimiwa Spika, Katika  kufanya  majadiliano ya bei za bidhaa muhimu Wizara ya  Biashara na Viwanda imeweza kufanya  mikutano  mbalimbali na Wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo ili kuweza  kujadiliana bei za bidhaa  muhimu kwa lengo la kuweka bei ambayo itakidhi kwa kila mfanyabiashara bila ya kumbana mwananchi. Mheshimiwa Spika, kutokana na majadiliano haya na wafanyabiashara, kumekuwepo na utulivu wa bei kwa bidhaa muhimu za chakula kama vile mchele, sukari, mafuta ya kupikia na unga wa ngano. Aidha, Wizara imeratibu uanzishwaji wa Kamati ya mashauriano ya kibiashara pamoja na vikao vyake. Kamati hio imeshirikisha wataalam kutoka ZFDA, ZBS, Idara ya Biashara na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ili kuweza kutoa ushirikiano pamoja na mashauriano ya kibiashara.

92.    Mheshimiwa Spika, Katika hatua nyengine ya kuhakikisha kuwa tunakuwa na eneo maalum la kudumu la kuonesha na kutangaza bidhaa za wajasiriamali hapa nchini, Wizara ya Biashara na Viwanda inaendelea kulitangaza eneo la Nyamanzi kwa ajili hiyo. Kwa kipindi hiki, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na kuandaa ripoti ya matumizi ya eneo pamoja na kupata gharama za uwekezaji wa Kiwanja hicho. Mradi huu unategemewa kutekelezwa kwa utaratibu wa mashirikiano baina ya Serikali na sekta Binafsi (PPP).

93.    Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kushirikiana na Tume ya Mipango pamoja na MKURABITA imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 210 walioko katika Wilaya ya Magharibi ‘B’, Unguja, na Wilaya ya Wete Pemba. Mafunzo hayo yamewalenga wajasiriamali kupata uwelewa kuhusiana na umuhimu wa kusajili biashara zao ili kuweza kutambulika kisheria na kuweza kupata fursa zinazopatikana katika kuendesha biashara kwa mfumo rasmi.
 Programu ndogo ya Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji
94.    Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji inasimamiwa na Idara ya Biashara (Kitengo cha Mizani na Vipimo) na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara. Program ndogo hii ilipangiwa jumla ya shilingi milioni 344.81 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 219.72 kwa ajili ya mishahara na kazi nyengine za kawaida sawa na asilimia 64 ya makadirio ya mwaka.
Uimarishaji Ushindani Halali wa Kibiashara
95.    Mheshimiwa Spika, Tume ya Ushindani Halali wa
Biashara na Kumlinda Mtumiaji (ZFCC) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria Namba 5 ya mwaka 2018. Lengo la Taasisi ni  kuhamasisha, kuimarisha na kulinda Ushindani halali wa Biashara na kumlinda Mtumiaji hapa Zanzibar kwa kuhakikisha kwamba kila muekezaji, mwenye kiwanda, mfanyabiashara na mjasiriamali anafanya shughuli zake bila ya kumkwaza mwengine kwa ajili ya ustawi wa uchumi wa Zanzibar.

96.    Mheshimiwa Spika, Katika kuzitekeleza shughuli zilizopangwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Tume ilipangiwa jumla ya TZS Shilingi milioni 145.0. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya TZS Shilingi milioni 92.8 ziliingizwa sawa na asilimia 64 ya matumizi kwa kipindi hicho.

97.    Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha ushindani halali wa kibiashara kwa maeneo ya biashara, Wizara ya Biashara na Viwanda imesimamia miungano ya Makampuni ambapo jumla ya taarifa za miungano sita (6) ya Makampuni zimefanyiwa kazi kwa kipindi hiki. Kati ya hizo, Mheshimiwa Spika, Taarifa za miungano kwa Makampuni matatu (3) zimekamilika na kuidhinishwa. Kadhalika, Tume imeendelea kutatua migogoro ya wafanyabiashara inayohusu ushindani wa kibiashara usio halali katika maeneo ya kughushi, kutumia jina na muonekano ambayo huathiri ushindani wa soko. Malalamiko hayo yamefanyiwa kazi na kutolewa maamuzi ya umiliki halali wa majina na muonekano wa biashara hizo.

98.    Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara na Viwanda inajukumu la kumlinda mtumiaji kutokana na bidhaa bandia zilizopo sokoni. Wizara kupitia Tume imefanya ukaguzi wa bidhaa mbali mbali katika maeneo ya biashara na bandarini.  Ukaguzi huo ulilenga kuangalia utambulisho wa bei na ubora wa bidhaa, maelezo ya bidhaa, dhamana kwa watumiaji,  bei elekezi kwa bidhaa zinazodhibitiwa, udhibiti wa bidhaa  bandia, bidhaa zisizo salama na Mikataba kwa Watumiaji. Katika ukaguzi huo jumla ya maduka ya kawaida 341, maghala 30, bekari 5 na maduka makubwa (Supermarket) 10 yamekaguliwa. Katika ukaguzi huo bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 17,217,000 zikiwa zimepitwa na muda wa matumizi zimekosa maelezo ya utumiaji na bidhaa bandia zilikamatwa na kuondolewa madukani. Bidhaa hizo ni pamoja na vyakula (nafaka na
juisi) na kemikali. Vile vile Tume kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeharibu bidhaa za kuchezea watoto zenye kemikali hatarishi zinazoweza kusababisha miripuko katika eneo la Unguja Ukuu Zanzibar.

99.    Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya biashara katika kukuza uchumi pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu unakwenda sambamba kwa mujibu wa mipango tuliojipangia, Tume imeandaa Muundo wa taasisi, muundo wa utumishi, Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) pamoja na kuwapatia mafunzo wafanyakazi ili kuhakikisha kuwa sekta ya biashara inaleta tija na maendeleo yaliyotarajiwa.
Ukaguzi wa Mizani na Vipimo

100. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara imefanya mapitio ya sheria na kanuni mbali mbali za biashara kwa lengo la kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa masuala ya biashara nchini. Mojawapo ya sheria muhimu iliyoandaliwa na kuwasilisha Serikalini ni Sheria ya Mizani na Vipimo ambapo sheria hiyo inapendekeza kuanzisha kwa Wakala wa vipimo ili kuongeza ufanisi katika kazi za uhakiki na ukaguzi wa vipimo katika maeneo yote yaliyoanishwa na sheria hii.

101. Mheshimiwa Spika, Mbali na ukaguzi wa mizani na vipimo vya mafuta katika vituo, magari, matangi na pampu, Wizara ya Biashara na Viwanda imeanza kuongeza kazi zake za ukaguzi na kwa sasa, ukaguzi unafanyika katika bidhaa zinazozalishwa katika viwanda mbali mbali vilivyopo hapa Zanzibar ili kuhakikisha vipimo vinavyotumika vinafanyika kwa usahihi. Katika ukaguzi wa vipimo hivi, jumla ya shilingi 60,370,000 zimekusanya ikiwa ni ada inayotokana na ukaguzi huo. Idadi ya huduma za ukaguzi zilizofanywa kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 inaonekana katika 

kiambatanisho namba 4.
 Programu ndogo ya Urahisishaji Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani

102. Mheshimiwa Spika, Program ndogo ya Urahisishaji Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani inatekelezwa na Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni (BLRC) na Baraza la Taifa la Biashara (ZNBC) ambapo ilipangiwa kutumia jumla ya shilingi bilioni 1.11  kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii ndogo imeingiziwa jumla ya shilingi milioni 622.91 kwa ajili matumizi ya kazi za kawaida, ruzuku na kazi za maendeleo sawa na asilimia 56 ya makadirio ya mwaka. Programu ndogo ya Urahisishaji Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani ina jukumu la kutekeleza huduma zifuatazo:-

Usimamizi wa Mamlaka zinazotoa Leseni

103. Mheshimiwa Spika, Huduma hii ilitekelezwa na Baraza la kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni ambalo lilipangiwa matumizi ya jumla ya shilingi milioni 745.5 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo shilingi milioni 345.5 kwa ajili ya kazi za kawaida na shilingi milioni 400 kwa kazi za maendeleo. Hadi kufikia Machi 2020, Baraza liliingiziwa jumla ya shilingi milioni 288.2 kwa matumizi ya kazi za kawaida na kazi za maendeleo sawa na asilimia 39 ya makadirio ya mwaka.

104. Mheshimiwa Spika, Baraza limefanya utafiti wa kutathmini Mfumo wa Utoaji leseni mwaka 2019. Utafiti umeonesha kwamba taratibu  za utoaji leseni zimepungua kutoka  hatua kumi (10) za awali na kufikia hatua tatu mpaka nne (3 – 4)  katika utoaji wa  leseni za utalii, usafiri, kazi za sanaa na wasanii, biashara, mazao ya kilimo na mifugo, vibali vya ujenzi na usalama wa chakula, vibali vya usafirishaji, uvuvi, nishati na  mawasiliano. Aidha, leseni zinazohusiana na uendeshaji wa hospitali, uvuvi wa bahari kuu, huduma za bandari  na uwekezaji zinatumia hatua nne mpaka tano (4 -5) katika utoaji wa leseni na vibali. Vile vile, utafiti unaonesha kwamba leseni za utalii, usafiri, kazi za sanaa na wasanii, biashara, mazao ya kilimo na mifugo, vibali vya ujenzi na usalama wa chakula zinatolewa ndani ya siku moja (1).

105. Mheshimiwa Spika Katika kuhakikisha usimamizi wa Mamlaka zinazotoa leseni unasimamiwa ipasavyo, Baraza imefanya vikao vinne (4) vya Baraza na vikao viwili (2) vya Kamati na kujadili ripoti za utekelezaji, mapitio ya sheria, mapitio ya ada na tozo za leseni na huduma nyenginezo
kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu ambao unaimarisha mfumo wa upatikanaji wa leseni. Aidha, Vikao vitatu (3) vya majadiliano vya sekta binafsi na Mamlaka vimeitishwa ambavyo vilijadili mapitio ya ada na tozo za leseni na huduma nyenginezo ili kuhakikisha kwamba utaratibu wa utoaji leseni unaendana na Sheria ya kusimamia utoaji leseni na kanuni zake. Aidha, Wajumbe kumi (10) na wafanyakazi wa watano (5) wa Baraza wamepatiwa mafunzo yanayohusiana na mfumo wa utoaji leseni, sheria, kanuni za Baraza na urahisi wa ufanyaji biashara.

106. Mheshimiwa Spika, Katika kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji kazi, Baraza limefanya matengenezo ya vyombo vya usafiri, ununuzi wa huduma za umeme, mafuta na vifaa vya ofisi.
Uimarishaji wa Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

107. Mheshimiwa Spika, Katika juhudi za Serikali kuhakikisha kwamba inajenga Sekta binafsi iliyokuwa imara imeanzisha Chombo maalum ambacho kimeweka misingi ya kufanya majadiliano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Chombo hicho (Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar -
ZNBC) kilianzishwa na Sheria iliyopitishwa na Baraza lako Tukufu Namba 10 ya mwaka 2017. Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar lilipangiwa kutumia Jumla ya shilingi milioni 360.0kama ni ruzuku kwa kazi za kawaida ambapo hadi kufikia mwezi wa Machi, 2020 jumla ya shilingi milioni 334.71 zilipatikana sawa asilimia 93.

108. Mheshimiwa Spika, Naomba kuliarifu Baraza lako Tukufu kwamba Baraza liliratibu mikutano kumi ya Mabaraza ya Biashara katika Mikoa yote mitano ya Zanzibar. Aidha, vikao vitano vya Kamati Tendaji ya Baraza vilikutana kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika Jukwaa la Tisa la Biashara pamoja na kufanyika kwa mikutano ya Kamati za Baraza la Biashara. Baraza pia linaendelea kufanya mapitio ya Sheria Nam. 10 ya mwaka 2017, ili iweze kukidhi mahitaji mapya yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

109. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara na Viwanda imeandaa Mkutano wa Tatu wa Baraza la Taifa la Biashara ambao unatakiwa kufanyika mara moja kwa mwaka. Mkutano huo ulifanyika chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mkutano ulihudhuriwa na wajumbe wote kutoka Sekta ya Umma pamoja na wajumbe kutoka Sekta Binafsi. Aidha, baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Jukwaa la Kumi la Biashara lilifanyika na kuhudhuriwa na washiriki wasiopungua 350, kutoka katika Taasisi za Serikali, taasisi za Sekta binafsi, Mabalozi pamoja na waalikwa wengine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

110. Mheshimiwa Spika, Jukwaa la kumi la Biashara ambalo lilikuwa na Kauli mbiu isemayo “Maendeleo Endelevu ya Zanzibar Kupitia Uchumi wa Bahari (Buluu)” , lilikuja na maazimio 14. Maazimio hayo yalijikita katika maeneo ya uimarishaji wa ulinzi katika bahari kuu, kuandaliwe Sheria ambayo itaweka mfumo mzuri wa usimamizi na ufuatiliaji wa michango inayotolewa na wawekezaji na wafanyabiashara (CSR), kuanzisha Mkakati wa kupeleka huduma za kifedha ikiwemo matawi ya benki na ATM ndani ya kilomita 5 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja na wananchi, Serikali ifungue ‘refund account’ au iweke utaratibu mwengine ulio bora wa marejesho ya VAT kwa wafanyabiashara na maazimio mengine yanayohusu kodi.
 Mheshimiwa Spika,  Wizara imeanza kufuatilia utekelezaji wa maazimio hayo yaliyofikiwa katika Jukwaa hilo la Kumi la Biashara.
 Programu ndogo ya Usimamizi wa Usajili wa
Biashara na Mali
111. Mheshimiwa Spika, Huduma hii ilitekelezwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) ambayo ilipangiwa matumizi ya jumla ya shilingi milioni 820.9 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 na hadi kufikia Machi 2020, Wakala iliingiziwa jumla ya shilingi milioni 550.99 kwa matumizi yakiwemo ya kazi za kawaida na matumizi mengineyo sawa na asilimia 67 ya makadirio ya mwaka.

112. Mheshimiwa Spika, Lengo kuu la kuanzishwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) ni kufanya usajili wa biashara na mali ikijumuisha hati za mali ubunifu pamoja na usajili wa nyaraka mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofanya shughuli zao Zanzibar. Kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2019/2020, BPRA imeweza kusajili Kampuni 636, Majina ya Biashara 884,  Alama za biashara 519 na Nyaraka 791.

113. Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha uwezo wa watendaji wa kutekeleza majukumu ya kazi ikiwemo usajili, uhifadhi kumbukumbu na utoaji wa taarifa (information services) kwa kutumia TEHAMA, wafanyakazi 2 wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu katika fani ya “Tehama” na
“Intellecttual Property and Development Policy” (MIPD) na Wafanyakazi 2 wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi ya
“Umuhimu na wajibu wa ukusanyaji wa mapato” na “Audit Tax International”. BPRA imekamilisha rasimu ya awali ya mapitio ya sheria ya ufilisi (Insolvency) kwa sasa rasimu hiyo iko katika hatua ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili, rasimu ya sheria ya ubia (Partnership) pamoja na kufanya marekebisho ya sheria ya Usajili wa taasisi za biashara. Aidha, BPRA imeshiriki katika uzinduzi wa program mpya ya shahada ya pili ya Mali ubunifu (Intellectual Property) katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

114. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa kuhamasisha wananchi kufanya usajili wa kisasa wa kutumia mfumo wa usajili wa mtandao (Online Registration System), Wizara ya Biashara na Viwanda kupitia BPRA imetoa elimu kuhusu usajili wa mali bunifu, usajili wa dhamana za mali zinazohamishika na usajili wa taasisi za biashara kupitia ZBC-TV. Pamoja na kufanya mikutano na wadau ya kuhamasisha uingizaji taarifa kwa waliosajiliwa kabla ya kuanza kutumika mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao kwa Unguja na Pemba.
       
           PROGRAMU KUU YA VIWANGO NA TATHMINI YA UBORA:

115. Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Viwango na Tathmini ya Ubora inasimamiwa na Taasisi ya Viwango Zanzibar, inajumuisha Programu moja ndogo ambayo ni Viwango na Uthibiti wa Ubora. Programu hii ilipangiwa matumizi ya shilingi bilioni 2.72 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Hadi kufikia Machi 2020, programu hii imeingiziwa jumla ya shilingi bilioni 1.07  ambayo ni ruzuku ya mishahara ya kazi za kawaida na kazi za maendeleo sawa na asilimia 39 ya makadirio ya mwaka. Utekelezaji wa huduma zilizopangwa katika program ndogo niliyoitaja hapo juu ni kama ifuatavyo:

Uandaaji na Ukuzaji wa Viwango

116. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Viwango imeendelea na jukumu lake la kuandaa viwango ambapo jumla ya viwango 103 vimeandaliwa na kuidhinishwa sawa na asilimia 172 ya lengo la uandaaji viwango. Viwango hivyo ni pamoja
na viwango vya chakula 31, Uhandisi mitambo 11, vifaa vya ujenzi 3, Kemikali 29, Umeme 9, Mazingira 11, Utalii 3 na nishati 4. ZBS imeendelea na kazi yake ya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha ubora wa bidhaa ambapo sampuli 662 zimekusanywa na kupelekwa maabara kwa hatua za upimaji wa ubora. Matokeo ya ripoti hizo yameonesha  kwamba sampuli 528 zimekidhi vigezo, sampuli 60 zimebainika kutokidhi vigezo na sampuli 74 bado hazijapatiwa majibu.

Ukaguzi na udhibiti ubora

117. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Viwango imefanya ukaguzi wa bidhaa na imefanikiwa kutoa Vyeti vya ubora wa bidhaa 876 na magari yaliyotumika 34 kwa mfumo wa ukaguzi nje ya nchi (PVoC). Jumla ya shehena 2,155 za mizigo na gari 4,516 zimekaguliwa kupitia mfumo wa ukaguzi wa ndani ya nchi (DI). Aidha, shehena 120 za mafuta ya nishati zimekaguliwa, kati ya hizo shehena 42 za Dizeli, 37 za Petroli, 28 za mafuta ya taa na 13 za mafuta ya ndege (Jet A1). Katika hatua za kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na zinazoingia nchini zimezingatia viwango katika nchi yetu, ZBS imepokea maombi 24 ya Uthibiti Ubora wa bidhaa pamoja na matumizi ya alama ya ubora. Kwa kipindi cha Julai – Machi Taasisi imetoa leseni 7 za alama ya ubora kwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini na nje ya nchi na hatua za ufuatiliaji zinaendelea kwa maombi ya bidhaa zilizobakia.
Uthibiti wa Ubora wa Bidhaa
118. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mradi wa Maendeleo wa kuimarisha Taasisi yetu ya viwango, imefanya ununuzi wa vifaa vya maabara ya chakula na tayari vimeshafungwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya utumiaji wa vifaa hivyo. Hivyo, kufanya jumla ya maabara tatu zinazotoa huduma hapo eneo la Amani kukamilika. Aidha,awamu ya pili ya ujenzi wa Ofisi na Maabara katika eneo la Maruhubi unatarajiwa kuendelea baada ya kukamilisha taratibu za Zabuni. Kwa upande wa Pemba matengenezo ya Ofisi ya Mkoani na Chake Chake yamekamilika ikiwa ni pamoja na kuwekewa mazingira mazuri ya kiutendaji na kuanza kutoa baadhi ya huduma za msingi.
         
             SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA (ZSTC):

119. Mheshimiwa Spika, Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) lilifanyiwa mageuzi makubwa ya kiuendeshaji chini ya Sheria Namba 11 ya 2011, ambayo imelipa uwezo Shirika kukuza, kuendeleza na kusimamia sekta nzima ya karafuu pamoja na mazao mengine ya kilimo hususani mazao ya viungo, pamoja na kuanzisha Sheria ya Maendeleo ya Mfuko wa Karafuu Namba 2 ya mwaka 2014. Huduma zilizotekelezwa kwa mwaka 2019/2020 ni kama zifuatazo:
Uvunaji na Usafirishaji Karafuu:
120. Mheshimiwa Spika, Shirika liliendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika (Corporate Strategic Plan) ambao uliweka dhamira ya utekelezaji wa Mpango wa Mageuzi wa miaka 10 kuanzia 2011 hadi 2021. Kwa mwaka wa fedha 2019/20 Shirika lilijipangia kununua jumla ya tani 5,100 za karafuu ukilinganisha na mwaka 2018/2019 ambapo lilipanga kununua tani 3,000 na tani 1000 za makonyo. Hadi kufikia tarehe 31/03/2020 Shirika limenunua jumla ya tani 4,361.8 zenye thamani ya shilingi bilioni 61.0 na Makonyo tani 624.06 yenye thamani ya Shilingi milioni 926.2.

121. Mheshimiwa Spika, Shirika bado linaendelea kununua Karafuu kwa bei ya TZS 14,000, TZS 12,000 na TZS 10,000 kwa kilo za daraja la kwanza, pili na tatu. Aidha,kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Shirika limefanya mauzo ya tani 5,640 za karafuu zenye thamani ya USD 26,661,620 sawa na Shilingi bilioni 61.05 kwa nchi ya India na Singapore.

Uzalishaji wa Mafuta ya Makonyo na Mimea

122. Mheshimiwa Spika, Shirika limefanikiwa kuzindua mtambo mpya wa uzalishaji wa mafuta ya Mkaratusi katika kiwanda cha mafuta ya Makonyo na Arki za mimea Wawi Pemba. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 6/01/2020 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar. Vile vile, Shirika limefanikisha mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata majani makavu ya karafuu kwa ajili ya kupata mafuta kilichojengwa eneo la Mgelema huko Pemba na tayari kimeanza uzalishaji. Kiwanda hiki ni makubaliano ya mkopo nafuu baina ya ZSTC na Kampuni ya INDESSO ya nchini Indonesia.

123. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Kiwanda cha Makonyo kilijipangia kutumia jumla ya shilingi bilioni 1.0 hadi kufikia tarehe 31/03/2020 Kiwanda cha Makonyo kimetumia jumla ya shilingi milioni 539.3 sawa na asilimia 53.9 ya makadirio ya mwaka. Uzalishaji wa mafuta kwa Kiwanda cha Makonyo ni kama inavyoonekana katika Kiambatanisho namba 5.
          Mapato na Matumizi ya Shirika

124. Mheshimiwa Spika, Shirika lilipanga kukusanya shilingi bilioni 76.6  kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo mauzo ya mafuta ya mimea, ukodishaji wa ukumbi na nyumba za wageni pamoja na mapato kutoka Shamba la Mtakata. Hadi kufikia tarehe 31/03/2020 jumla ya shilingi bilioni 53.8  zimekusanywa kutoka kwa vyanzo hivyo vya mapato sawa na asilimia 70 ya makadirio ya mwaka.

125. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa matumizi, Shirika lilikadiria kutumia jumla ya shilingi bilioni 14.1 ikiwa ni gharama mbali mbali za uendeshaji, wakati matumizi halisi kwa kipindi cha Julai-Machi, 2019/2020 ni shilingi bilioni
7.1.
      
    Mradi wa PiliPili

126. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa mradi wa kuwapatia ajira vijana kupitia kilimo cha pilipili, Serikali iliunda Kamati Maalum ya kufanya tathimini ya utekelezaji wake. Baada ya uwasilishaji wa ripoti ya Kamati, Serikali ilitoa uamuzi wa kukabidhiwa mradi wa pilipili kwa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa uratibu na kuendelea na hatua za utekelezaji kwa kuzingatia kuwa walengwa wa Mradi huu ni Vijana.

5 CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MALENGO KWA MWAKA 2019/2020:

127. Mheshimiwa Spika, Pamoja na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa malengo na majukumu mbali mbali ya Wizara kwa mwaka 2019 /2020, pia zipo changamoto zilizoathiri utekelezaji wa malengo yaliyopangwa katika sekta ya biashara na viwanda. Miongoni mwa changamoto hizo  ni kama ifuatavyo:-
i. Kushuka kwa bei ya Karafuu katika soko la Dunia ii. Vikwazo vya kibiashara katika soko la Tanzania Bara iii. Kutokuwepo na eneo la kuandaa Tamasha na maonesho mbali mbali hapa Zanzibar.
iv. Kutokuwa na mfumo rasmi wa ukusanyaji wa Takwimu za Biashara na Viwanda.

128. Mheshimiwa Spika, Kupitia Baraza lako, Wizara inawaomba wadau wote wa biashara na viwanda wakiwemo wananchi, Serikali, Sekta binafsi, Jumuiya mbali mbali kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hizi ili kuwapa unafuu wananchi wa Zanzibar. 

6        PROGRAMU ZA WIZARA KWA MWAKA 2020/2021

129. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara ya Biashara na Viwanda inatarajia kuendeleza azma yake ya kukuza Viwanda kama inavyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 – 2020 ibara namba 84 (a, b mpaka h). Pia maazimio yaliyomo katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUZA III 2016 – 2020) pamoja na miongozo ya Viongozi Wakuu wa nchi yetu. Maeneo mengine makuu yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya Biashara, utafutaji wa masoko na usaidizi wa wajasiriamali na wazalishaji wadogo wadogo.

130. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Biashara na Viwanda inatarajia kutekeleza shughuli mahsusi zifuatazo katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 kama vipaumbele vyake:-
i.         Kuyaendeleza na kuyapima maeneo ya viwanda, Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kuandaa Mpango wa matumizi (Master Plan) na upembuzi yakinifu (feasibility study) kwa eneo la Dunga ili wawekezaji waliokuwa tayari kuwekeza wapimiwe na kuanza ujenzi. Pamoja na kufikisha miundombinu ya umeme, maji na kukata barabara za ndani. Vile vile Wizara, itaendelea kuyapima maeneo mapya yatakayoanishwa na Kamisheni ya Ardhi kwa ajili ya viwanda.

ii.        Kuendeleza ujenzi wa Ofisi na Maabara za ZBS kwa awamu ya pili
 Mheshimiwa Spika, Kutokana na kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Ofisi na maabara, Wizara itaendelea na awamu ya pili ili kukamilisha ujenzi wa maabara na Ofisi za ZBS Maruhubi. Aidha, Kuimarisha utekelezaji wa Mfumo wa Ubora ndani ya ZBS (QMS) kwa kutumia kiwango cha ISO 9001:2015 na kuweka mfumo wa TEHAMA utakaorahisisha na kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa kazi.

iii.      Kuliendeleza eneo la Nyamanzi na kuandaa Matamasha mbalimbali
Mheshimiwa Spika, Eneo la  maonesho la Nyamanzi limewekwa katika orodha ya Miradi ya kuendelezwa kwa kushirikiana na sekta binafsi (PPP), Wizara inakusudia kuliandaa eneo hilo kwa kufanya Tathmini ya kimazingira na kijamii (ESIA) pamoja na kulisafisha eneo hilo. Pia, Wizara inatarajia kuongeza vifaa vya kufanyia matamasha ikiwemo matenti na magazebo.

iv.      Kuandaa Mfumo wa Kitaifa wa Usajili wa Biashara na Utoaji leseni na kuunganisha Mamlaka za utoaji leseni (NOBS)
Mheshimiwa Spika, Ili kuendelea kurahisisha ufanyaji biashara hapa Zanzibar, Wizara itaimarisha mfumo maalum wa kitaifa wa usajili wa Biashara na Utoaji wa leseni (NOBS) pamoja na kuziunganisha Mamlaka za utoaji leseni. Mfumo huu wa Tehama utatoa taarifa na huduma muhimu za usajili, uwekezaji na leseni au vibali vinavyotakiwa na wawekezaji na wafanyabiashara.

v.        Kuanzisha na Kuimarisha Wakala wa Vipimo na Mizani
Mheshimiwa Spika, Kutokana na kupitishwa kwa sheria na kuanzishwa kwa Wakala wa vipimo, kwa mwaka 2020/2021, Wizara inatarajia  kuanzisha taasisi hiyo na kuiimarisha kwa kuipatia vifaa vya kutendea kazi kama vile wafanyakazi, kanuni ambazo zitaongoza ufanyaji kazi pamoja na sehemu ya Ofisi.
vi.      Kuimarisha Tume Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji:
Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha mazingira mazuri ya ushindani halali wa kibiashara na kumlinda mtumiaji, Wizara itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji kazi kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na sheria ya ushindani halali wa kibiashara na kumlinda mtumiaji. Pia, kufanya chunguzi, utafiti, kusikiliza mashauri yanayoathiri Ushindani katika soko na Miungano (Merger).
vii.     Kuimarisha Wakala wa Kusimamia wazalishaji wadogo wadogo na wa kati:
Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kuendeleza ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya SMIDA iliopo Maruhubi, kuanzisha kituo cha usarifu wa mazao ya kilimo (Agribusiness Innovation Center) huko Kizimbani na Maruhubi kwa kushirikiana na PASS.
viii.   Kuimarisha Takwimu za Biashara na Viwanda: Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kuweka mfumo maalum utakaotumika kukusanya takwimu za Biashara na Viwanda ambazo zitatumika katika mipango ya maendeleo na mengine ya Serikali na sekta Binafsi hatimae zitawasilishwa kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali.
ix.      Kuwaendeleza wajasiriamali na wazalishaji wadogo:
Mheshimiwa Spika, Kupitia program ya kuwaendeleza wajasiriamali na wazalishaji wadogo wadogo na wa kati, Wizara itatoa mafunzo na mikopo kwa wazalishaji wadogo wadogo kutoka Halmashauri na Miji ya Zanzibar na makundi maalum ya vijana na wanawake ili kuwapatia mitaji na kuweza kujiajiri.
x.        Kuendeleza usarifu wa mwani:
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia ZSTC inatarajia kuanzisha kiwanda cha kusarifu mwani kwa kushirikiana na wawekezaji kutoka Indonesia. Kiwanda kinatarajiwa kuwepo katika eneo la Chamanangwe Pemba.

xi.      Kuendeleza na kufanya tafiti mbalimbali za biashara na viwanda
Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2020/21, Wizara itaendelea na utafiti wa Mazingira Mazuri ya Biashara (Easy of Doing Business), Utafiti wa bidhaa kwa soko la AGOA na utafiti wa bidhaa za madawa asilia.
xii.     Uimarishaji wa Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Serikali
Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kuendeleza mashirikiano haya kwa kuyasimamia na kuyaendeleza Mabaraza ya Biashara ya Mikoa, kuandaa Mkutano wa nne (4) wa Baraza la Biashara na Jukwaa la Kumi na moja (11) la Biashara kwa mwaka wa fedha 2020/21.

xiii.   Kwa upande wa Shirika la Biashara la Taifa, linatarajia kununua Karafuu tani 4,000 na Makonyo tani 800 kwa msimu wa mwaka 2020/21, kuendelea uzalishaji wa mafuta ya Makonyo na mimea mengine pamoja na kuratibu uzalishaji wa wa mafuta ya karafuu kwa kufunga vinu sita vya kusindika majani  makavu ya karafuu kwa upande wa Pemba.

6.1 Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2020/2021

131. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/21, Wizara ya Biashara na Viwanda imepangiwa matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 23.570. Kati ya fedha hizo Jumla ya shilingi bilioni 8.77 zimetengwa kwa ajili ya Matumizi ya kazi za kawaida na Mishahara na shilingi bilioni 14.80 kwa kazi za Maendeleo. Fedha za maendeleo ni pamoja na Shilingi bilioni 4.6 tunazotarajia kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa programu ya kuwaendeleza wajasiriamali na wazalishaji wadogo wadogo na wa kati ( Khalifa Fund ).

Mheshimwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/21 Wizara ya Biashara na Viwanda imepanga kutekeleza miradi mikuu mitano (5) ya maendeleo ambayo ni: - Kuimarisha maendeleo ya viwanda, Kuimarisha Mazingira bora ya biashara, Kuimarisha Taasisi ya Viwango Zanzibar, Mfumo wa utowaji leseni kwa maendeleo ya sekta binafsi na kuimarisha wajasiriamali.

132. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara ya Biashara na Viwanda itaendelea kutekeleza program kuu nne (4) na program ndogo kumi (10). Programu kuu hizo kama zifuatavyo:
i.           Programu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ii.       Programu ya Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali iii.          Programu ya Ukuzaji na Uendelezaji Biashara
iv.         Programu ya Viwango na Uthibiti Ubora

 PROGRAMU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

133. Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda imegawika katika Programu ndogo tatu kwa mujibu wa huduma ambazo inazitoa. Program hizo ndogo ni kama zifuatazo:
i.        Utawala na Uendeshaji wa shughuli za Wizara ya
Biashara na Viwanda; ii.         Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti za Wizara; na iii. Uratibu na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara Pemba
134. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Utawala na Uendeshaji wa shughuli za Wizara ya Biashara na Viwanda ambayo inatekelezwa na Idara ya Uendeshaji na Utumishi itakuwa na jukumu la kutoa huduma ya usimamizi wa rasilimali watu na huduma za kiofisi kwa ujumla pamoja na ununuzi wa vifaa. Ili kutekeleza majukumu yake, programu hii ndogo imepangiwa matumizi ya shilingi bilioni 2.29 kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021.

135. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa program ndogo ya Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti za Wizara ambayo utekelezaji wake utasimamiwa na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, itakuwa na jukumu la uandaaji na uibuaji wa sera na tafiti za Wizara, uandaaji na utekelezaji wa mipango
ya Wizara pamoja na usimamizi wa takwimu za Biashara na Viwanda. Katika kutekeleza huduma hizo, programu ndogo ya uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti imepangiwa matumizi ya shilingi milioni 579.08 kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

136. Mheshimiwa Spika, Program ndogo ya Uratibu na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara Pemba ambayo inaratibu shughuli za uendeshaji wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa upande wa Pemba imepangiwa matumizi ya shilingi milioni 652.94 kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

137. Mheshimiwa Spika, Ili kuweza kutekeleza shughuli zilizopangwa katika Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwaka 2020/2021, naliomba Baraza lako tukufu kuidhinisha matumizi ya shilingi bilioni 3.53 kwa program hii kuu.
     
   PROGRAMU YA MAENDELEO YA VIWANDA NA UJASIRIAMALI

138. Mheshimiwa Spika, Programu kuu ya Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali imegawika katika Programu ndogo mbili kwa mujibu wa huduma ambazo inazitoa. Program hizo ndogo ni kama zifuatazo: i. Ukuzaji  Viwanda ii. Maendeleo ya Ujasiriamali

139. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ukuzaji Viwanda itakuwa na jukumu la kutoa huduma ya Uimarishaji wa Sekta ya Viwanda ikiwemo kusimamia ujenzi wa maeneo maalum ya viwanda (Industrial Parks), Ujenzi wa Makao Makuu ya Ofisi ya SMIDA, pamoja na kuimarisha kitengo cha inteligensia ya viwanda ambapo utekelezaji wake utasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Viwanda na SMIDA. Ili kutekeleza huduma hii, programu hii ndogo imepangiwa matumizi ya shilingi bilioni 3.61 kwa mwaka 2020/2021.

140. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa programu ndogo ya Maendeleo ya Ujasiriamali ambayo ina jukumu la kutoa mafunzo, msaada na mikopo kwa wajasiriamali, Ili kutekeleza huduma hii, programu hii ndogo imetengewa shilingi bilioni 9.17 kwa mwaka 2020/2021.

141. Mheshimiwa Spika, Ili kutekeleza majukumu ya Program kuu ya Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali kwa mwaka 2020/2021, naomba Baraza lako tukufu liidhinishe matumizi ya shilingi bilioni 12.78 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za programu hii kuu.
        PROGRAMU YA      UKUZAJI     NA     UENDELEZAJI BIASHARA
142. Mheshimiwa Spika, Programu ya tatu itakayotekelezwa na Wizara kwa mwaka 2020/2021 ni Ukuzaji na Uendelezaji Biashara. Kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa malengo yake, programu hii imegawanyika katika Programu ndogo nne
(4) kama zifuatavyo:
i.           Ukuzaji Masoko na Usafirishaji ii. Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji iii.          Urahisishaji Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani iv.         Usajili wa Biashara na Mali
143. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Ukuzaji Masoko na Usafirishaji itakuwa na jukumu la kutoa huduma za uimarishaji wa mazingira mazuri ya biashara, kuongeza fursa za masoko pamoja na urahisishaji biashara ambapo utekelezaji wake utasimamiwa na Idara ya Biashara. Ili kutekeleza huduma hizo, programu ndogo ya Ukuzaji wa Masoko na Usafirishaji imetengewa shilingi milioni 856.30 kwa mwaka 2020/2021.

144. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa programu ndogo ya Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji ambayo itakuwa na jukumu la kuimarisha ushindani halali wa kibiashara na kumlinda mtumiaji kwa kuendelea kutoa huduma za ukaguzi na uhakiki wa vifaa vya mizani, vipimo, ukaguzi wa biashara na maghala pamoja na ushajihishaji na utoaji wa elimu kwa watumiaji, ambapo utekelezaji wake utasimamiwa na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara na Idara ya Biashara (baadae Wakala wa Vipimo na Mizani). Ili kutekeleza huduma hizo, naliomba Baraza lako tukufu liidhinishe matumizi ya shilingi milioni 376.87 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

145. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Urahisishaji Biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani itakuwa na jukumu la kutoa huduma za usimamizi wa mamlaka zinazotoa leseni kwa kufanya utafiti na kuweka vigezo vinavyohusu leseni chini ya Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji leseni. Aidha, Baraza la Taifa la Biashara litasimamia uimarishaji wa majadiliano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa kuandaa majukwaa mbalimbali ya biashara nchini. Ili kutekeleza huduma hizo zilizopangwa chini ya Programu hii ndogo, naliomba Baraza lako tukufu liidhinishe matumizi ya shilingi bilioni 1.22 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

146. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Usajili wa Biashara na Mali ambayo itakuwa na jukumu la usimamizi wa usajili wa biashara na mali kwa Mfumo wa kielektroniki na kuimarisha mifumo ya usajili wa biashara na mali. Ili kutekeleza huduma hizo, naliomba Baraza lako tukufu liidhinishe shilingi milioni 867.7 kwa mwaka 2020/2021.

147. Mheshimiwa Spika, Ili kutekeleza huduma zilizopangwa katika Programu kuu hii ya Ukuzaji na Uendelezaji Biashara kwa mwaka 2020/2021, naliomba Baraza lako tukufu liidhinishe jumla ya shilingi bilioni 3.32 kwa program hii kuu.
      
  PROGRAMU YA VIWANGO NA TATHMINI YA UBORA

148. Mheshimiwa Spika,  Programu  kuu  ya nne itakayotekelezwa na Wizara kwa mwaka 2020/2021 ni Viwango na Tathmini ya Ubora. Kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa malengo yake, programu hii imepangiwa kuwa na programu ndogo moja ya Viwango na Uthibiti wa Ubora ambayo itakuwa na huduma za Uandaaji na Ukuzaji wa Viwango pamoja na huduma za Tathmini ya Ubora wa Bidhaa. Utekelezaji wake utasimamiwa na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS). Ili kutekeleza shughuli zilizopangwa katika programu hii, naliomba Baraza lako liidhinishe shilingi bilioni 3.94 kwa mwaka wa fedha 2020/2021  kwa program hii kuu.

149. Mheshimiwa Spika, Taarifa kamili ya Wizara hii imeelezwa katika kitabu cha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Bajeti inayotumia Programu (PBB) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 – 2022/2023 kutoka ukurasa wa R01 mpaka ukurasa wa R018.
SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA – ZSTC

Shughuli za Shirika kwa mwaka wa fedha                                              
2020/2021
150. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/ 2021, Shirika la Biashara la Taifa linatarajia kutekeleza shughuli kuu zifuatazo;
i.          Ununuzi wa karafuu tani 4,000 na makonyo tani
800 ; ii. Kuongeza uzalishaji wa mafuta ya mimea kwa kuimarisha shamba la Mtakata, mashamba ya mkaratusi na kukiimarisha Kiwanda cha Makonyo;
iii.       Kuimarisha vitega uchumi vya Shirika vikiwemo; jengo la Madungu, Malindi na eneo la Saateni.
iv.       Kukamilisha taratibu za uanzishwaji wa kiwanda cha kusarifu mwani.

Ununuzi na Mauzo ya Karafuu

151. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/2021, bei ya kununulia Karafuu kutoka kwa wakulima inatarajiwa kutobadilika kutoka TZS 14,000 kwa kilo moja daraja la kwanza, TZS 12,000 kwa daraja la pili na TZS 10,000 kwa daraja la tatu. 
152. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020 /2021, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa limeidhinisha matumizi ya Jumla ya shilingi bilioni 73.67 katika kutekeleza kazi za kawaida, Maendeleo pamoja na ununuzi wa karafuu na makonyo.

7        SHUKRANI:
153. Mheshimiwa Spika, Mafanikio ya Wizara yaliyopatikana ni matokeo ya mashirikiano makubwa ya Wajumbe wa Baraza hili chini ya uongozi wako mahiri. Ninakushukuru wewe binafsi, Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Baraza
na Wajumbe wote kwa ushauri na michango mliyotupatia katika kipindi cha utekelezaji wa bajeti. Shukrani zangu pia ziende kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo Mheshimiwa Mwinyihaji Makame Mwadini, Mwakilishi wa Jimbo la Dimani, wajumbe na Makatibu wote wa Kamati hiyo kwa ushauri na miongozo waliyoitoa katika mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Biashara na Viwanda na hatimae kuridhia mapendekezo haya yawasilishwe katika Baraza hili.

154. Mheshimiwa Spika, Mafanikio ya kiutendaji yaliyojitokeza katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ni matokeo ya ushirikiano mkubwa uliopatiwa Wizara ya Biashara na Viwanda kutoka kwa wadau mbali mbali wa ndani na nje ya nchi yetu. Kwa madhumuni ya kutambua mchango mkubwa wa Wadau mbali mbali kwa Wizara, naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa nchi na taasisi za ndani na nje zifuatazo; Jamhuri ya Watu wa China, India, Jumuiya ya Ulaya (EU),USAID, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Shirika la Kimataifa la Tasnia ya Malibunifu (WIPO), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (World Bank), Shirika la Biashara Duniani (WTO), TANTRADE, Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH), Zanzibar Seaweed Cluster Initiative (Zasci), Milele Foundation, Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) na Wafanyabiashara wote wakubwa, wadogo na Wawekezaji wa Viwanda.

Aidha, napenda kuishukuru Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mashirikiano yao kwenye shughuli mbali mbali tulizofanya.

155. Mheshimiwa Spika, Napenda nichukue fursa hii kwa mara nyingine tena kuwapongeza kwa dhati viongozi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kazi kubwa yenye ufanisi mzuri wanayoifanya kila siku licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali, ni matarajio yangu kwamba wataongeza juhudi zao ili kuzidisha ufanisi kwa kuwahudumia wananchi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Kadhalika, napenda kuwapongeza wafanyakazi wote walioshiriki katika maandalizi ya Hotuba hii kwa kazi nzuri waliyoifanya, nawaombea dua njema katika kazi zao za sasa na zijazo.

156. Mheshimiwa Spika, Naomba niwashukuru wafanyabiashara na wenye viwanda wote wakubwa, wakati na wadogo kwa juhudi zao kubwa za kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia huduma mbali mbali pamoja na bidhaa muhimu za chakula, nguo, vyombo vya moto, na vifaa vya ujenzi.  Nawaomba waendelee kushirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kufanya kazi pamoja kwa lengo la kuimarisha biashara na kutoa huduma bora kwa wananchi.

8 MAOMBI YA FEDHA KWA PROGRAMU KWA MWAKA
WA FEDHA 2020/2021
         
Mapato ya Serikali:

157. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara ya Biashara na Viwanda imepanga kukusanya jumla ya shilingi bilioni 2.36. Mapato hayo yatakusanywa kutoka vianzio tofauti kama inavyoonekana katika 


Jadweli Namba 3:                                                                                                                            
Mapato ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2020 - 2021
Mapato ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2020 - 2021                    
KIFUNGU
MAELEZO
MAKADIRIO 
R0104
Idara ya Biashara na Ukuzaji Masoko 
154,400,000
1422014
Ukaguzi wa Mezani na Vipimo
154,400,000



R0109
Tume ya Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji
250,000,000
1422077
Malipo ya kazi za biashara
250,000,000



R0105
Idara ya Uendeshaji na Utumishi
197,268,000
1422078
Malipo kwa ajili ya Ukodishwaji wa Maeneo ya kibiashara
197,268,000



R0106
Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali
709,827,719
1146002
Ada ya Utunzaji Urithi
1,200,000
1422030
Alama za Biashara
350,700,000
1422031
Uandikishaji wa Makampuni
234,327,719
1422032
Uandikishaji wa Majina ya Biashara
72,400,000
1422034
Ujira wa kutengeneza nyaraka
51,200,000



R0107
Taasisi ya Viwango Zanzibar
976,000,000
1112008
Malipo ya usimamizi viwango
976,000,000



R0101
Afisi Kuu-Pemba
80,301,281
1422014
Ukaguzi wa Mezani na Vipimo
42,901,281
1422078
Malipo kwa ajili ya Ukodishaji wa Maneneo ya kibiashara
12,000,000
1422031
Uandikishaji wa Makampuni
2,200,000
1422032
Uandikishaji wa Majina ya Biashara
1,200,000
1422034
Ujira wa kutengeneza nyaraka
22,000,000
Jumla Kuu

2,367,797,000

Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020
          Matumizi:
158. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa matumizi ili Wizara ya Biashara na Viwanda iweze kutekeleza programu zake ilizojiwekea kwa mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako tukufu  liidhinishe matumizi ya jumla ya shilingi 23,569,700,000  kwa programu nne (4) kama inavyoonekana katika Jadweli Namba 4:

Jadweli Namba 4:                                                                                                                 
Maombi ya Fedha (TZS Mil)                                                              

Maombi ya Fedha (TZS Mil)                                                   


Geresho (Code)
Programu Kuu/Programu ndogo
Makadirio  2020 - 2021 (mil)
PR0101
Uendeshaji wa Uratibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda 
3,526.98
SR010101
Utawala na Uendeshaji wa Wizara ya Biashara na Viwanda.
2,294.98
SR010102
Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti za Wizara
579.07
SR010103
Uratibu na Utekelezaji wa shughuli za Wizara Pemba
            652.93


PR0102
Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali
12,782.15
SR010201
Ukuzaji wa Viwanda
3,612.75
SR010202
Maendeleo ya Ujasiriamali
9,169.40


PR0103
Ukuzaji na Uendelezaji wa Biashara
3,316.77
SR010301
Ukuzaji wa Masoko na Usafirishaji 
856.30
SR010302
Ushindani Halali wa Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji
376.87
SR010303
Urahisishaji biashara na Ukuzaji Biashara za Ndani
1,215.90
SR010304
Usajili wa Biashara na Mali
867.70


PR0104
Viwango na Tathmini ya Ubora 
3,943.80
SR010401
Viwango na Uthibiti Ubora
3,943.80


 JUMLA KUU
23,569,700



Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020

9        HITIMISHO:

159. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo niliyatoa, naomba waheshimiwa wajumbe wa Baraza lako tukufu kuidhinisha mapendekezo ya kukusanya mapato ya shilingi bilioni 2.36 kutokana na huduma zinazotolewa na Wizara. Aidha ili Wizara ya Biashara na Viwanda iweze kutekeleza shughuli zilizopangwa kwa mwaka wa fedha 2020/20221, naomba Wajumbe wa Baraza lako tukufu kuidhinisha matumizi ya shilingi 23,569,700,000 kwa fungu la R01.
160. Mheshimiwa Spika, Nakushukuru wewe binafsi, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza lako pamoja na wananchi kwa kunisikiliza.
161. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja.
  
10VIAMBATANISHO

Kiambatanisho Namba 1.                                                                                                            

Michango na kodi zilizokusanywa na Mamlaka za mapato ZRB,  TRA na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (TZS).

ZRB
TRA
ZSSF
Jumla
ZMCL
596,650.14
507,363.30
117,662.54
1,221,675.98
ZSFL
1,278,409.60
278,814.03
230,093.71
1,787,313.34
ADPL
186,723.84
95,100.00
75,600.00
 357,423.84
JUMLA
2,061,783.58
881,277.33
423,356.25
3,366,413.16
 Chanzo: ADPL, ZSFL, ZMCL April 2020



Kiambatanisho Namba 2.                                                                                                      

Matumizi ya Fedha kwa kipindi cha Julai 2019 – Machi 2020                                  

 S/N 
Programu Kuu 
Fedha
Zilizotengwa kwa  Mwaka wa
Fedha
2019/2020 TZS  
Fedha Zilizopatikana kwa Kipindi cha Miezi
Tisa (Julai - Machi,
2019/2020) TZS  
Asilimia ya
Fedha
Iliyopatikana
 PRO1 
Uendeshaji na Uratibu wa  Wizara ya
Biashara 
2,992,621,800
2,313,908,658
77

Utawala na Uendeshaji wa Wizara 
2,139,511,316
1,735,995,907
81

Uratibu wa Mipango, Sera na Utafiti 
367,121,800
235,553,221
64

Uratibu na Utekelezaji wa




shughuli za Wizara Pemba 
485,988,684
342,359,530
70
 PR02 
 Maendeleo ya
Viwanda na
Ujasiriamali 
6,853,911,000
1,083,451,605
16

Ukuzaji Viwanda 
3,286,514,000
1,062,342,353
32

Maendeleo ya Ujasiriamali 
3,567,397,000
21,109,252
1
 PR03 
Ukuzaji na
Uendelezaji wa
Biashara 
3,026,067,200
1,787,057,972
59

Ukuzaji Masoko na Usafirishaji 
754,857,200
393,450,075
52

Ushindani Halali wa




Kibiashara na Kumlinda Mtumiaji 
344,810,000
219,716,550
64

Urahisishaji wa Biashara




na Ukuzaji biashara za ndani 
1,105,500,000
622,906,000
56

Usajili wa Biashara na Mali 
820,900,000
550,985,347
67
 PR04 
Viwango na Tathmini ya Ubora. 
2,724,800,000
1,066,438,052
39

Viwango na Udhibiti Ubora. 
2,724,800,000
1,066,438,052
39




40

 JUMLA KUU  
15,597,400,000
6,250,856,287

Chanzo: Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020

!Kiambatanisho Namba 3.


Baadhi ya Viwanda na hatua mbali mbali za uanzishaji wake kwa kipindi 2019/2020.
NA
M
JINA LA KIWANDA
MAHALI
BIDHAA
HALI YA KIWANDA
MUELEKEO/MATEGEMEO

1.
Kiwanda cha Chumvi
Chamanang we Pemba
Chumvi


Uzalishaji mdogo umeanza  katika sehemu nyengine kwa muda
Ulipaji wa fidia kwa wenye vipando umekamilika na  ujenzi wa kiwanda unaendelea 

2.
Kiwanda Cha Mwani
Chamanang we Pemba
Karajina
Site plan ya kiwanda
hichi imeshaandaliwa
Utaratibu wa mashirika ya Serikali kushirikiana kujenga
kiwanda hicho ndio utakaotumika  

3.
Kiwanda cha Mafuta ya Majani ya Karafuu
MgelemaPemba
Mafuta ya majani
makavu ya karafuu
Kiwanda kipya tayari kimejengwa na tayari kimeanza uzalishaji
Kiwanda kimetoa ajira za moja kwa moja 15 kwa Wananchi wa Pemba na ajira nyingi zisizo za moja kwa moja.

4.
Kiwanda cha Maziwa
Chamanang we Pemba
Maziwa
Bado wazalishaji samli ya ng’ombe wanaendelea na uzalishaji katika eneo lao la awali liliopo kisiwani kwa
Binti Abeid
Hatua za kuwashajiisha kufanya uzalishaji katika eneo lililotengwa la viwanda
Chamanangwe zinaendelea.

5.
Kiwanda cha Bomba
za Plastic
Maruhubi
Mabomb
a
Mwekezaji anaendelea na ujenzi wa kiwanda
Kiwanda kinatarajia kuanza kazi mwisho wa mwaka 2020

6.
Kiwanda cha Tungule
na Pilipili
ShakaniUnguja
Tungule
na Pilipili
Kiwanda kipya kinatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi wa April
Kiwanda kitatumia malighafi kutoka kwa wakulima wetu hapa hapa Zanzibar 

7.
Kiwanda cha
Vifungashio
Uzini-
Unguja
Vifungas hio
Kiwanda kinafanya kazi
Bidhaa zake tayari ziko sokoni


8.
Kiwanda cha
Vifungashio
NyamanziUnguja
Vifungas hio(Mifuk o ya karatasi)
Kiwanda kinafanya kazi
Bidhaa zake tayari ziko sokoni


9.
Kiwanda cha
Vifungashio
Wilaya ya kati-Unguja
Vifungas hio
Kiwanda tayari kimeanza na uzalishaji wa mifuko
(carrier bags)
Bidhaa zake tayari ziko sokoni Zanzibar na Tanzania bara. Matarajio ni kulifikia soko la Comoro.

10.
Kiwanda
cha Vibiriti
Wilaya ya kati-Unguja
Vibiriti
Mwekezaji
anaendelea na kulifanyia kazi jambo hili ili kuona kama ataendelea na uwekezaji huo au atawekeza kwenye mradi mwengine 
Ukosefu wa umeme wa uhakika ni tatizo kubwa kwa sasa 

11.
Kiwanda cha minofu ya kuku
Wilaya ya Kati-Unguja
kuku
Usajili wa kampuni
BPRA na ZIPA tayari Hatua za kupatiwa hati ya ardhi (land lease) zinaendelea kazi
Mradi huu utajumuisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha chakula cha kuku pamoja na
chinjio la kisasa

12.
Kiwanda cha Chakula cha Mifugo
Wilaya ya Kati-Unguja
chakula cha mifugo
Usajili wa kampuni
BPRA na ZIPA tayari Hatua za kupatiwa hati ya ardhi (land lease) zinaendelea kazi
Kitaanza kazi baada ya kumaliza taratibu zote.

13.
Kiwanda cha kutotolea Vifaranga vya Kuku
Wilaya      ya
Kati
Vifarang
a             vya
kuku
Usajili wa kampuni BPRA na ZIPA tayari Hatua za kupatiwa hati ya ardhi (land lease) zinaendelea
kazi
Wizara imefanya mkutano wa wadau ili kupata maoni na kukusanya sheria za taasisi mbali mbali zitakazosaidia wawekezaji wa mradi huo
- Memorandum of






understanding (MOU) kwa ajili ya kuweka makubaliano ya pamoja kati ya Wizara ya kilimo na wawekezaji wa mradi huo ili kuhakikisha mradi unaendelea
14.
Kiwanda cha Ushoni 
Buyu-
Unguja
Nguo
Mazungumzo bado yanaendelea baina ya Serikali na Muwekezaji kutoka China.
Mwekezaji                anaendelea
kufanyia kazi jambo hili
15.
Kiwanda cha kuzalisha Vitambaa
Basra-
Textile Mills-
Chumbuni
Unguja
Nguo
Awamu ya kwanza ya mashine tayari zimeshawasili kiwandani. Shehena iliyobaki ilitarajiwa kuwasili ndani ya mwezi wa April 2020 
Kiwanda kinatarajiwa kuanza uzalishaji kwa majaribio kabla ya mwezi Agosti 2020. Hatua zimesita kutokana Covid 19 imechelewesha kufika kwa shehena iliyobaki pamoja na wataalamu.
16.
Kiwanda cha Kukaushia
Dagaa
Fungurefu
Mkokotoni
Dagaa na Samaki
Kampuni ya Uvuvi ya ZAFICO imeshaanza taratibu za awali za kumtafuta Mshauri elekezi atakaebuni michoro ya kiwanda hicho.
Timu iliyofanya tathmini imetoa mapendekezo kwa bodi juu ya kufanya uhakiki wa kampuni zilizojitokeza kabla ya kufanya maamuzi ya kumpa tenda mmoja kati ya hao.
17.
Kiwanda
cha Mafuta ya mkaratusi
Wawi-
Pemba
Mafuta
Kiwanda kimekamilika na kiko tayari kwa uzalishaji
Kiwanda kinasubiri malighafi kutoka shambani
18.
Kiwanda cha kusarifu
Ndimu
Chwaka
Sirapu ya Ndimu
Jengo la Kiwanda limeshamalizika,
imebaki kuweka milango na
Madirisha
Mashine imeshafika na uzalishaji utaanza mara moja ujenzi utakapokamilika
19.
Kiwanda cha Kusarifu Tungule
Mtule Paje
Tomato sauce
Kinafanya kazi
Kiwanda kimeanza uzalishaji
Kiambatanisho Namba 4.                                                                                                                         
Huduma ya Ukaguzi                                          

Eneo la Ukaguzi
Jumla
Mezani ndogo
2,146
Mezani kubwa (Platform)
27
Mezani (Weigh bridge)
0
Mita za Depot (Flow Meter)
50
Pampu za kuuzia mafuta
307
Fillers
0
Magari ya kusambaza mafuta
20
Matangi ya mafuta
19
Uthibitisho wa tanks (Certification)
0
Usajili wa Kampuni za mafuta
0
Bidhaa za Viwandani
zilizofungashwa
6


Chanzo:  Wizara ya Biashara na Viwanda, 2020
Kiambatanisho Namba 5.  Hali ya Uzalishaji Kwa Mwaka 2019/2020
Aina ya Mafuta
Lengo
2019/2020 (Kg)
Uzalishaji Halisi (Kg)
Thamani (TZS)
Makonyo
46,875.0
6,003
194,473,188.00
Mchaichai
150.0
142.546
22,847,500.00
Mdalasini
37.5
2.0
650,000.00
Mrehani
18.75
4.25
1,381,250
Mkaratusi(manukato)
750.0
156.5
12,520,000.00
Mkaratusi(madawa)
243.75
86.0
6,880,000.00
Majani ya mkarafuu
375
369.2
29,536,000.00
Unga wa  Karafuu
0
4,561.5
232,216,842.00
Chanzo: Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC), 2020
Mhe. Zubeir Ali Maulid akizinduwa rasmi Tamasha la Sita la Biashara lililofanyika Januari 2020 katika Viwanja vya Maisara
Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara - Tanzania Bara, akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara kuhusu Kliniki ya Biashara, Januari 2020.
Muonekano Mpya wa Kiwanda cha nguo cha Basra Textile Ltd kilichopo Chumbuni baada ya ukarabati
Mashine za kiwanda kipya cha Basra Textile zilizowasili Nchini hivi karibuni
Maafisa wakiwa katika kazi za upimaji wa vifaa vya elektroniki ndani ya Maabara za ZBS - Amani
Mfanyakazi wa Kiwanda cha Ushoni (ZQTL) kilichopo Amani akiwa katika ukataji wa Barakoa
Bidhaa za Chumvi inayozalishwa kutoka Pemba na kusarifiwa na Kampuni ya Swahili Coast Salt Ltd
Miongoni mwa muonekano wa bidhaa za Chumvi katika ujazo na ladha tofauti

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.