Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP26, Glasgow, Scotland

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP26  unaoendelea katika Mji wa  Glasgow, Scotland leo tarehe 02 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula pamoja na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo mara baada kuhutubia katika Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP26 unaoendelea katika Mji wa Glasgow, Scotland.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro wakati akielekea kwenye Mkutano maalumu wa Viongozi Wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP26  unaoendelea katika Mji wa  Glasgow, Scotland leo tarehe 02 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano huo maalumu wa Viongozi Wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP26  unaoendelea katika Mji wa  Glasgow, Scotland leo tarehe 02 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali Wanawake katika Mkutano huo maalumu wa COP 26 unaoendelea katika Mji wa  Glasgow, Scotland leo tarehe 02 Novemba, 2021. 

PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.