Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu
maswali bungeni jijini Dodoma leo tarehe 9 Aprili, 2029 wakati wa Kikao cha
Pili cha Mkutano wa 19 wa Bunge.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
amesema Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT).
Mhe. Khamis amesema
hayo bungeni jijini Dodoma leo tarehe 9 Aprili, 2025 wakati akijibu swali la
Mhe. Bakar Hamad Bakar (Baraza la Wawakilshi) aliyetaka kujua kwa kiasi gani
Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia Serikali
ya Muungano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Akiendelea
kujibu swali hilo, Mhe. Khamis ameeleza kuwa kupitia fedha hizo, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na SJMT imeendelea kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ametaja miradi
iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume Pemba,
Barabara ya Tunguu hadi Makunduchi, Chakechake hadi Wete kupitia kwa Binti
Abeid na ujenzi wa Skuli, Hosptali na Masoko.
Amesema miradi
inayotekelezwa Zanzibar imewasaidia wananchi wa pande zote mbili za Muungano kushiriki
na kuinua hali zao za kiuchumi pamoja na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
”Sheria ya
Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 imeweka utaratibu wa namna SMZ inavyopaswa
kunufaika na mikopo, dhamana na misaada kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,” amesema.
Pamoja na
kupongeza hatua ya Serikali ya kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha hizo, Mhe.
Bakar katika swali lake la nyongeza alitaka kujua kama Serikali haioni haja ya kupitia
na kuboresha utaratibu mpya kwa mgawanyo wa fedha kutoka kwa wadau wa
maendeleo.
Katika majibu ya
Serikali, Naibu Waziri Khamis amesema utaratibu wa mgawanyo wa fedha upo kwa
mujibu wa sheria na umewek wazi kuwa Zanzibar inanufaika kwa asilimia 4.5 na Tanzania
Bara asilimia 95.5.
Ameongeza kuwa katika
kuhakikisha Muungano unaendelea kuwa imara Serikali zote mbili zimekuwa
zikifanya vikao bado vikao vinakaliwa ili kuna namna ya kuboresha kuhakkikisha.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis bungeni jijini Dodoma leo tarehe 9 Aprili,
2029 wakati wa Kikao cha Pili cha Mkutano wa 19 wa Bunge.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande jibu maswali
bungeni jijini Dodoma leo tarehe 9 Aprili, 2029 wakati wa Kikao cha Pili cha
Mkutano wa 19 wa Bunge.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde bungeni jijini
Dodoma leo tarehe 9 Aprili, 2029 wakati wa Kikao cha Pili cha Mkutano wa 19 wa
Bunge.
No comments:
Post a Comment